Shule
za watoto walemavu ikiwemo shule ya matumaini iliyopo chini ya jeshi la
wokovu -Salvation Army zinakabiliwa na changamoto mbalimbali hususani
upatikanaji wa fedha za kutosha katika kuendesha shughuli zake shuleni
hapo.
Wakizungumza jijini Dar es Salaam katibu wa huduma za jamii wa
jeshi hilo na mkurugenzi wa shule hiyo amezitaja baadhi ya changamoto
zinazo wakabili ni pamoja na chakula na matibabu kwa watoto hao ambao ni
walemavu.
Nao baadhi ya wafadhiri ambao wamejitokeza kuwafadhiri watoto hao
wamesema kuwa watoto hao wanaitaji upendo na kwamba endepo watapatiwa
elimu ya kutosha wanauwezo wa kuwa kama watoto wengine.
No comments:
Post a Comment