TTCL

EQUITY

Monday, December 7, 2015

Nisha; Nimepania kuliteka soko la mitindo nchini

Msanii wa filamu nchini Tanzania, Salma Jabu 'Nisha'
Msanii wa filamu nchini Tanzania, Salma Jabu ‘Nisha’

Msanii wa filamu nchini Tanzania, Salma Jabu ‘Nisha’, amesema kuwa licha ya kuwa vizuri katika tasnia ya filamu na uchekeshaji anampango wa kufungua kampuni yake ya mavazi ambayo itakuwa inawavalishsa mastaa mbalimbali.
Msanii huyo amedai kuwa ili kudhihirisha kuwa yupo makini na kazi yake ameanza rasmi kumvalisha model Hamisa Mobeto, ili kuonesha uwezo wake katika fani hiyo.

Msanii wa filamu nchini Tanzania, Salma Jabu 'Nisha' katika pozi
Msanii wa filamu nchini Tanzania, Salma Jabu ‘Nisha’ katika pozi

Amedai kuwa mitindo ni kitu ambacho alikuwa akikipenda tangu akiwa mdogo yaani kabla hata hajafirikia kuwa msanii na ndio maana ameamua kuudhihirishia ulimwengu kuwa kazi hiyo pia anaweza kuimudu vyema.

Amesema kuwa ameanza na kumvalisha Hamisa Mobeto, lakini lengo lake ni kuja kuwa na kampuni inayohusu ubunifu hasa vitu vya asili ili kuweza kujitangaza na kuitangaza nchi ya Tanzania.
Ameongeza kuwa ameamua kujikita kwenye mitindo, nguo za kike, nywele pamoja na vitu mbalimbali vya urembo.

No comments:

Post a Comment