TTCL

EQUITY

Monday, December 7, 2015

UREMBO WA NYUMBA NI PAMOJA NA MUONEKANO MZURI WA JIKO LAKO.


Mara nyingi watu wanapoongelea kupamba nyumba wanazingatia zaidi sebule na sehemu zingine na kulisahau kabisa jiko.
Jikoni pia linafaa kupendeza ili kumpa mpishi hamu ya kupika na hata kumpa mlaji hamu ya kula Chakula kama  kikipikwa katika mazingira safi na mazuri.Kwa upande mwingine hata wewe mpishi unapata nguvu ya kuwepo jikoni endapo utaweka jiko lako katika mazingira mazuri.

jiko 2
Wengi hawapambi na kutengeneza jiko kwa madai ya kuwa na gharama kubwa ya maboresho hayo ili hali wageni huwa awafiki jikoni lahasha , Ukweli ni kwamba hiki ni kisingizio kisichofaa hata kidogo kwani kupamba au kutengeneza jiko zuri si lazima utumie gharama kubwa hata  kuweka mpangilio mzuri wa jiko ni urembo tosha.

jiko 1
Kuna mambo madogo unayoweza kufanya ili kupendezesha jiko lako na kulipa mvuto kwa kufanya haya:
1.Mpangilio wa vitu: Ili jiko livutie ni lazima liwe na mpangilio mzuri na wenye nafasi, Kupanga huku kunahusisha meza za jikoni,vyombo kabatini,ndoo,majiko,friji na kila kikaacho jikoni. Jitahidi vyombo vyote vikae ndani ya kabati la vyombo na kama kabati ni dogo na vyombo ni vingi basi  tunza ndani ya Boksi au mabeseni makubwa ili mradi tu visisambae jikoni.
2.Matumizi ya  rangi zinazo ng’ara: Rangi zinazong’ara hupendezesha sana jiko,ni vyema kununua vitu vyenye rangi za kung’ara ili kung’arisha zaidi jiko.Rangi hizo ni kama Kijani,njano,nyekundu,bluu,nyeupe ,orenji na zingine.
3.Urembo wa aina mbalimbali: Ni vyema kuwa mbunifu na kutumia urembo wa aina mbalimbali kupendezesha jiko.Unaweza tumia vyungu vya aina mbalimbali na rangi mbalimbali kwa kuvipanga juu ya kabati au sehemu nyingine yoyote.
4.Vyombo vizuri: Vyombo vizuri hulipa jiko mvuto,nunua vyombo vyenye maumbo na rangi mbalimbali.mfano badala ya kununua sahani za duara kila mara unaweza nunua sahani za pembe nne au zenye umbo la yai.
6.Ondoa vitu usivyotumia: Ni vyema ukaondoa jikoni kitu chochote usichotumia,kwani vinachukua nafasi na kujaza jiko bila sababu.watu wengi hupenda kutunza vitu wasivyotumia kama majiko mabovu,vyombo vibovu na kadhalika

jiko 4
Tabia hii  ni mwanzo wa uchafu jikoni,na uwepo wa mende na panya.Pia hufanya mtu asinunue vitu vipya kwa kujipa moyo kua anavyo,wakati ukweli ni kwamba  alivyonavyo ni vibovu na havifai.

No comments:

Post a Comment