Maternity wear ambazo zinaweza kuvaliwa ofisini na ukaonekana vizuri. Hapa kuna baadhi ya nguo ambazo zinafaa kuvaliwa ofisini kwa mtu ambaye hapendelei kuvaa suruali. Kuna maternity sketi ambazo tumboni kunakuwa na belti kubwa la mpira la kukuwezesha kuvaa bila kupata tabu. Vile vile unaweza kuvaa magauni yenye mikono midogo mizuri au yasiyo na mikono na kisha kuvaa na koti dogo zuri au vijisweta vidogo na kukufanya ukaonekana mrembo na mwenye kupendeza.