Msanii
wa sanaa za Maonesho Vanensia Shule, ambaye pia ni Mkufunzi wa Chuo
kikuu cha Dar es salaam upande wa sanaa na Filamu akielezea jinsi Sanaa
inavyoweza kumkomboa kijana, na kutoa mifano ya baadhi ya wasanii
walioanzia chini na sasa wanamafanikio makubwa,jana tarehe 4.12.2015.
Baadhi ya vijana wakionesha ishara ya ushindi.
Alphonse
Matata ambaye anajihusisha na kilimo pia Mjasiliamali kupitia ufugaji
wa nyuki akielezea safari yake ya mafanikio ,na kuwashauri vijana
wasingoje kuajiliwa bali wawe wabunifu na kujiunga katika ujasiliamali, jana tarehe 4.12.2015.
MC Suhaila Thawer akiendelea kutoa utaratibu wa wazungumzaji.
Mjasiliamali
Maarufu na Mtoa ushauri wa biashara na mambo mbalimbali James
Mwang'amba, alitoa Historia ya Maisha yake na kutoa siri tatu za
mafanikio ambazo ni kuwa na maono ya maisha bora ya baadae, kujifunza
kwa kupitia njia mpya ya Teknolojia mfano youtube na kuwa na mtu ambaye
unahisi unaweza ukajifunza kwake.
Baadhi ya vijana wakifuatilia Kongamano hil.
Aliyekuwa
nahodha wa timu ya Taifa ya wanawake 2002-2003 na kuchezea mpira timu
hiyo kwa Miaka 15 mpaka anastaafu mwaka huu Esther Chabruma akielezea
namna mchezo wa Mpira wa Miguu ilivyoweza msaidia mpaka hapa alipofikia
na kuwasihi vijana wasikate tamaa maana kila jambo lina wakati wak.
Baadhi ya vijana wakiwa wanasikiliza kwa makini vijana wenzao wakielezea safari zao za mafanikio.
Rais
wa Serikali ya wanafunzi Chuo kikuu cha Dar es salaam Kitaponda Ahadi,
akielezea kuhusu elimu na changamoto alizo zipata wakati wa akiwa Shule
mpaka ndoto yake ilivyotimia ya kuja kusoma chuo kikuu na kuwa kiongozi,
amewasihi vijana wenzake wasikate tamaa wafanye bidii katika masomo
watafikia malengo.
Major
Mbuya mtaalam wa kuendesha Baiskeri na mwanzilishi wa waendesha
Baiskeri Tanzania, akielezea jinsi ubunifu ulivyo msaidia mpaka sasa
amefanikiwa
Hassan
ally kijana mjasiliamali akieleza namna alivyoweza kubadilisha taka na
kuwa Bidhaa ambayo inaweza kutumika tena kwa matumizi mengine pia,
ameelezea mpango wake wa kuanza kujenga nyumba kwa kutumia bei nafuu.
Vijana
mbalimbali wamejitokeza katika kongamano la msafara kusikiliza baadhi
ya vijana wenzao ambao wametoa historia zao kuhusu walipotokea mpaka
wamefanikiwa kufika hapo walipofikia na kuwatia moyo vijana wengine
wasikate tamaa kwa sababu mafanikio yapo.
Msafara
ambao unalenga kuibua na kurudisha ndoto za vijana katika sekta zote
kwa kutambua kuwa kila eneo lina mchango mkubwa katika mafanikio na
maendeleo ya vijana. Wazungumzaji tofauti tofauti walijikita katika
maeneo makuu yafuatayo Sayansi na Teknolojia,Kilimo, Biashara, Sanaa na
usanii, Elimu, Uongozi, Michezo, utunzaji Mazingira, haki sawa za
kijinsia pamoja na harakati.
Maeneo
hayo yalikuwa ni nguzo kuu ya kufanya vijana kuwa na fursa ya
kukabiliana na changamoto za kimaisha katika kufikia mafanikio na
malengo yao. Katika safari hii ya Msafara matukio mbalimbali yatafanyika
ikiwemo kuwaleta vijana wa rika moja wenye umri wa miaka 15-24 ili
kuwaleta kwa pamoja wapate kujifunza kutoka kwa wengine waliofanikiwa,
wenye fani mbalimbali/Taaruma zao, hii itawajengea ujasili wengine
katika kufikia mafanikio yao.
Progamu
hii inaendeshwa na muungano wa Mashirika na Makundi Matano yaliyopo
hapa Tanzania ikiwa ni pamoja na DARUSO, YouthCAN, NGAO YOUTH na Young
Feminist Forum na inaratibiwa na Oxfam Tanzania, msafara itakuwa ni moja
ya fursa kwa vijana kutangaza na kuonesha ubunifu wao na mafanikio
waliyofikia kimaisha ingawa kuna changamoto na vikwazo mbalimbali.
Safari ya msafara itaendelea Ifakara mkoani Morogoro tarehe 12.12.2015
No comments:
Post a Comment