TTCL

EQUITY

Tuesday, December 1, 2015

Burkina Faso yapata Rais mpya

 Roch Marc Christian Kabore
Rais Mteule alikua Waziri Mkuu wa zamani katika utawala wa Blaise Compaore 
 
Roch Marc Christian Kabore ameshinda uchaguzi mkuu wa nchi hiyo, kwa mujibu wa tume ya uchaguzi.
Waziri Mkuu huyo wa zamani alipata alisimia 53 nukta tano hivyo amepata ushindi wa moja kwa moja, kwa kuzoa zaidi ya asili mia 50.
Huu ndio uchaguzi mkuu wa kwanza tangu maandamano yaliyomuondoa madarakani Rais wa miaka mingi Blaise Compaore.
Uchaguzi Mkuu ulitarajiwa kufanyika mwezi uliopita lakini ukacheleweshwa na jaribio la mapinduzi ambalo halikufaulu hapo mwezi Septemba.
Bwana Compaore anaishi uhamishoni katika nchi jirani ya Ivory Coast.

 Rais mteule Roch Marc KaboreRais Mteule {Katikati/mwenye miwani} aliwahi kuhudumu kama Waziri Mkuu 
 
Mshindani mkuu wa bwana Kabore, Zephrine Diabre alipata asili mia 21 ya kura. Yeye ni Waziri wa zamani wa Uchumi na Fedha.
Duru zinasema bwana Diabre amekubali kushindwa na kumpongeza Rais mteule,Roch Marc Christian Kabore.

No comments:

Post a Comment