TTCL

EQUITY

Monday, December 7, 2015

Benki ya Dunia imepongeza Rais Magufuli kimapato

Ikiwa ni siku ya 32 tu tangu aingie madarakani, Benki ya Dunia (WB) imepongeza Rais John Magufuli kwa kuongeza mapato na kupunguza matumizi ya serikali ya Tanzania
Benki ya dunia imesema inaridhishwa na utendaji kazi wa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dr.John Pombe Magufuli na kwamba inaunga mkono jitihada zake za kubana matumizi, kuongeza mapato na kuhakikisha huduma za kijamii zinawafikia watanzania wote na kwamba iko tayari kushirikiana na Tanzania katika miradi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na upanuzi wa bandari ya dar es salaam,ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kimataifa.
Hayo yamebainika katika kikao kilichomkutanisha rais Dr.John Pombe Magufuli na mwakilishi mkazi wa benki ya dunia Bi.Bella Bird ikulu jijini dar es salaam ambapo katibu mkuu wa wizara ya fedha Dr. Servacius Likwelile amesema benki hiyo inaridhishwa na utendaji kazi rais Dr.Magufuli na kwamba iko tayari kushirikiana na Tanzania katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni pamoja na upanuzi wa bandari ya Dar es Salaam.
Dr.Likwelile ameendelea kufafanua maeneo ambayo yamegusiwa katika mazungumzo baina ya rais Dr.Magufuli na mwakilishi huyo mkazi wa benki ya dunia Bi.Bella Bird.
Takribani miradi zaidi ya ishirini na tisa imefadhiliwa na benki hiyo ya dunia nchini ambapo kiasi cha dola bilioni nne zimekwishatolewa na benki hiyo hapa nchini.

No comments:

Post a Comment