TTCL

EQUITY

Friday, June 19, 2015

JUKWAA LA WATANGAZA NIA



Mwaka 1997 Watanzania waliambiwa dhahabu ndio mwarobaini wa umasikini. Mwaka 2015 Watanzania wanaambiwa Gesi Asilia ndio mwarobaini, Nchi kama Nigeria, Angola, Equatorial Guinea nazo zina utajiri mkubwa wa mafuta na gesi. swali Je,  vyote hivi vimeweza kuwa suluhisho la umasikini katika nchi zao?
Karibia wagombea wote wa CCM waliojitokeza hadi sasa hakuna aliyehusika kusema anamikakati gani ya kuhakikisha analeta chachu ya maendeleo katika kufufua viwanda vilivyo poteza fursa za maelfu ya ajira, na ongezeko la uchumi wetu.
rushwa sio sababu pekee ya kuporomoka kwa shilingi ya Tanzania, na wala sio sababu ya kutokuwepo kwa fursa za ajira sekta ambayo inauwezo wa kutengeneza uchumi wetu kukua na kushika kasi katika nchi zinazo kuwa kiuchumi duniani.

No comments:

Post a Comment