TTCL

EQUITY

Monday, March 9, 2015

STORY IN THE CORDIAL: CHADEMA WADAI CCM WANAPANGA KUMUUA DK SLAA

Mabere Marando na Benson Kigaira
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Mabere Marando (kushoto) na Mkurugenzi wa Operesheni ya Uchaguzi wa Chadema, Benson Kigaira


MABERE Marando- Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Madendeleo (Chadema), amefichua mawasiliano ya siri yanayofanywa na vyombo vya dola dhidi ya chama, na mkakati wa kumdhuru Katibu Mkuu, Dk. Willibroad Slaa. Anaandika Sarafina Lidwin.
 
       Amesema kuwa Idara ya Usalama wa Taifa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa, Philip Mangula, wamekuwa wakimtumia Khalid Kagenzi-mlinzi binafsi wa Dk. Slaa ili kurekodi na kuvujisha taarifa za vikao vya siri vya Chadema.
 
      “Kama chama tumelalamikia sana serikali ya CCM kwa matumizi mabaya ya vyombo vya dola dhidi yetu. Sasa tumebaini wanatumia vijana wetu kunasa taarifa zetu.
 
       “Kagenzi kwa miaka miwili tumebaini amekuwa akitumika kupeleka taarifa za Chadema kwa usalama wa taifa. Amekiri hilo kwa maandishi na kutaja namba za watu wa usalama anaowasiliana nao,” amesema.
 
       Marado alimtuhumu Mangula kuwa imebainika anawasiliana na Kagenzi ikiwa ni pamoja na kumtumia fedha mara mbili, Julai 24 na Desemba 4 mwaka jana, kupitia simu yake ya Vodacom (anaitaja).
 
        Kwa mujibu wa Marandu, mlinzi huyo alipobanwa zaidi alieleza mkakati uliokuwa ukipangwa na watu hao wa kumwekea Dk. Slaa sumu kwenye chakula au kinywaji.
 
Amesema kuwa wamebaini nyendo hizo hivi karibuni baada ya mlinzi huyo kuonekana akipanda katika gari ya afisa usalama wa mkoa wa Kinondoni lenye namba za usajili T213 ARS, akiwa nalo afisa msaidizi.
 
Marando amefafanua kuwa watamfikisha Kagenzi polisi ili achunguzwe na hatua zaidi zichukulie, lakini akakataa kuweka hadharani namba za simu na majina ya maafisa usalama aliodai wako zaidi ya 22.
 
         Amesema kuwa pia wamenasa taarifa za maofisa hao za kumtumia Kagenzi muda wa maongezi zaidi ya shilinigi milioni saba kwa nyakati tofauti.

No comments:

Post a Comment