TTCL

EQUITY

Monday, March 2, 2015

KAMPUNI YA HUAWEI YAONGOZA KATIKA TEKNOLOJIA YA MAWASILIANO DUNIANI 'ICT'



Hawa watu ni kiboko na dunia imeendelea kuwaelewa kila siku zinavyosogea yani, nilikua sijui kama HUAWEI iliingia kwenye bidhaa bora 100 za dunia mwaka 2014 tena ikiwa bidhaa pekee ya China kuingia kwenye hiyo top 100.

Nilialikwa kuja hapa Barcelona Hispania kuhudhuria maonyesho ya bidhaa za simu duniani ambapo HUAWEI pia wanashiriki, nimekutana na mapya mazuri wakati bado maonyesho haya yanaendelea ndio maana nikasema nikushirikishe na wewe mtu wangu yasikupite haya mazuri kutoka HUAWEI.
h2

Kama ulikua hujui HUAWEI ni kampuni inayoongoza katika teknolojia ya mawasiliano (ICT) duniani ambapo kwenye hivi vitu vipya walivyovitambulisha March 1 2015 ni Huawei MediaPad X2TalkBand B2TalkBand N1, pamoja na LTE CarFi vinatumia teknolojia ya kisasa zaidi kuruhusu watumiaji wake kuunganishwa popote walipo.


h3
Imagine sasa hivi wamekusogezea mpaka hii LTE CarFi, Internet mpaka kwenye gari
Katika kile ambacho dunia nzima inashangaa, Huawei wamezidi kurahisisha maisha kwa kuzindua CarFi 4G LTE. Hivi ni vifaa ambavyo vina kasi hadi 150 Mbps na vitaigeuza gari yako kuwa ‘hotspot’ ya kutawanya internet na kuunganisha vifaa hadi kumi kwa wakati mmoja ambapo hapa Hispania, Huawei wameweka vifaa hivi kwenye magari 400 na vimeonyesha kufanya kazi kwa ubora wa hali ya juu kabisa.
Nakumbuka wakati vinatambulishwa vipya mkurugenzi mtendaji wa Huawei Consumer Business Group Richard Yu amesema “kufuatia mafanikio ya Huawei MediaPad X1 na kurithi muundo wa kipekee wenye kioo kikubwa zaidi, MediaPad X2 inadhihirisha imani na utekelezaji wa ahadi yetu katika kutengeneza vifaa vyenye ubora wa hali ya juu tukitumia teknolojia na uvumbuzi wetu mpya
h4
Huawei MediaPad ni ya kipekee sana kwani ni Phablet (phone+tablet) yenye 8 Core, kiooHD na wembamba , yenye kutumia laini mbili na hivyo kuifanya kuwa simu ya kwanza duniani ikiwa na teknolojia ya LTE.

Yu akasema tena “Ikiwa ni aina ya pili ya MediaPad, Huawei MediaPad imejikita kwenye matumizi matano yenye umuhimu zaidi kwa watumiaji. Matumizi hayo ni pamoja na ubora wa simu zinazopigwa, application za mitandao ya kijamii, manunuzi mtandaoni, video na picha zenye kuongeza tija kwa mtumiaji, tuna imani kuwa MediaPad itaendelea kuongeza ari kwa watumiaji kupitia muundo wake wa kipekee na uwezo wake wa hali ya juu.”
h5
Unaambiwa Huawei ni kampuni namba moja ya teknolojia ya mawasiliano (ICT) duniani, ikiwa na makao makuu yake huko Shenzhen China, wana maabara na vituo 16 vya utafiti wa teknolojia mpya kwenye nchi mbalimbali duniani ikiwamo Ujerumani, Sweden, Marekani, Ufaransa, Italia, Urusi, India na China.


h6
Katika vitu ambavyo vimenishawishi kwa asilimia kubwa pia ni hii, unapofanya mazoezi au kutembea nayo ni nyepesi na wameitengeneza kisasa zaidi haiwezi kuwa mzigo kwako.
h7
Kwa upande wa Talkband B1, hivi ni vifaa vipya ambavyo huvaliwa mkononi vikiwa ni muunganiko wa ‘headset’ na uwezo wa kupima shughuli za mwili kama vile mazoez, pia Huawei wamezindua Talkband N2 ambazo hufanya kazi sawa na Talkband B1 isipokuwa huwa na sauti zenye ubora zaidi kwa wale wapenzi wa muziki waliodata na muziki.

h8
Vifaa vya Huawei hutumika na moja ya tatu ya watu wote duniani kwenye nchi zaidi ya 170. Mwaka 2014, Huawei ilikuwa ni kampuni ya tatu kwa uzalishaji na usambazaji wa ‘smartphones’ duniani.

h9
h10

No comments:

Post a Comment