Takriban
watoto 80 waliookolewa katika kambi ya kundi la Boko Haram nchini
Cameroon hawawezi kukumbuka majina yao kulingana na afisa mmoja
aliyewatembelea.
Watoto hao walipatikana katika kambi kazkazini mwa Cameroon mnamo mwezi Novemba.
Kundi la Boko Haram kutoka Nigeria limepanua mashambulizi yake hadi nchini Cameroon.
Wapiganaji hao wanajaribu kusimamisha taifa lenye uongozi wa kiislamu kazkazini mashariki mwa Nigeria.
Wanadhibiti miji kadhaa na vijiji katika jimbo hilo na hivi majuzi waliahidi kuiga mfano wa kundi la Islamic State ambalo limeteka eneo kubwa la Syria na Iraq.
No comments:
Post a Comment