TTCL

EQUITY

Saturday, December 6, 2014

Rose MhandoAfunguka kuhusu kutekwa kwake: Nilitekwa na Bastola na Kupelekwa Porini Kufanya Mapenzi

NYOTA wa Nyimbo za Injili Bongo, Rose Mhando (pichani)amefungukia eneo fupi la maisha yake magumu ambapo alisema amewahi kutekwa kwa bastola na mwanaume mmoja, akampeleka msituni ambako alimlazimisha kuwa naye kimapenzi lakini akadunda

Akizungumza na Gazeti la Amani juzi, Rose alieleza kwa machungu kwamba, tukio hilo lilimkuta hivi karibuni mjini Dodoma ambako ndiko kwenye makazi yake ya kudumu.Ilikuwa ni katika mahojiano ya kukiri kwake (my confession) ambapo Rose aliweka bayana kuhusu mazingira ya tukio hilo la kushangaza.


MSIKIE MWENYEWE
“Dunia ina mambo mengi sana ndugu zanguni, wengine wema, wengine waovu. Mimi nakumbuka siku moja kuna mwanaume ambaye nilikuwa na ukaribu naye.“Huyu bwana, ana jina kubwa sana Dodoma. Alinichukua kwenye gari kwa ajili ya kunisaidia mambo fulani maana alikuwa ananisaidia katika kazi zangu.


“Nilishangaa kumuona anapeleka gari nje ya mji,  nikamuuliza tunakwenda wapi, akasema tulia utajua.
“Sikuwa nimemuwazia ubaya, hivyo nilitulia lakini matokeo yake akanipeleka hadi porini ambako alikutana na watu wengine, naamini walikuwa wasaidizi wake.


“Naamini ulikuwa mpango kabambe. Wale watu wakaniweka chini ya ulinzi na kunifunga kamba kisha wakanioneshea mtutu wa bastola,” alisema Rose huku akisisitiza ni tukio ambalo hawezi kulisahau.


AAMBIWA KISA
Rose aliendelea kudai kuwa, mpaka hapo hakuwa amejua kisa lakini akiwa amekutana macho na mdomo wa bastola. Ndipo akaambiwa kuwa, anatakiwa kuwa chini ya himaya ya kimapenzi ya mwanaume huyo la sivyo siku zake zilikuwa zinahesabika.“Niliona ni jambo la ajabu, kwani mwanaume kumtaka mwanamke ni mpaka silaha na kutishia kuua?” alihoji staa huyo mkubwa wa gospo.


AKUBALI YAISHE
Rose aliendelea: “Kwa pale nilikubali kwamba niko tayari kuwa mtu wake lakini nikamwambia tukirudi mjini tukae tuongee kwa kirefu, akakubali.“Tulifika mjini nikiwa najisikia kuumwa sana maana wale wasaizidi wake walikuwa wakinisulubu kwa kunipigapiga pia ile kamba niliyofungwa ilichangia kunipa maumivu makali.”


AKACHA KUKUTANA
Rose alisema walipofika mjini walipanga kukutana baadaye ili wayaongee lakini yeye akakacha kutokea kwenye kikao, hivyo akaenda polisi (hakutaja kituo) ambako alifungua jalada la uchunguzi.“Nimekuwa nikisita kumwanika kwa jina huyo mwanaume kwani yupo na ni adui yangu mkubwa. Naishi kwa tahadhari kubwa sana, naamini siku nikimtaja ataniua.


“Mbaya zaidi najua mambo yake mengi, mabaya kwa mazuri lakini mabaya ni mengi sana kwani hata wakati ananisaidia kuhusu kazi zangu alinitenda maovu mengi, nimemwachia Mungu.”


KWA NINI AMEAMUA KUSEMA?
“Nimeamua kusema ili moyo wangu uwe mweupe, nimekuwa nikiwaza siku hadi siku kuhusu lile tukio, ni kumbukumbu mbaya sana kwangu, lakini kwa kukiri kwangu huku sasa nitakuwa na amani.”
Amani: “Polisi walichukua uamuzi gani?”


Rose: “Walisema wanafanya uchunguzi wa kina lakini sijawahi kuambiwa walifikia wapi!”
Amani: “Baada ya kuingia mitini jamaa hajawahi kukutumia meseji ya kukutishia maisha?”
Rose: “Hapana, alijua nimekwenda polisi.”


Amani: “Unadhani ni kwa nini alikuteka hadi msituni, kwa nini asikwambie tu kawaida mjini?”
Rose: “Alishawahi kuanza hizo dalili za kunitaka nikamwonesha sitaki, nilimwambia nataka kazi kwake na si mapenzi. Mimi najua fedha ndiyo jeuri yake.”                   
Amani: “Ana familia?”


Rose: “Ana mke na watoto.”
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime alipotafutwa hakuweza kupatikana kuzungumzia ishu hiyo.