TTCL

EQUITY

Tuesday, December 2, 2014

Mwimbaji wa nyimbo za injili amekamatwa na polisi akiendesha harambee mtaa kwa mtaa

MWIMBAJI  wa  nyimbo  za  injili maarufu nchini Tanzania ambaye ni mlemavu  wa  mkono mmoja Mwinjilisi Joseph  Nyuki maarufu kwa jina la Balozi wa  Yesu amejikuta  mikononi  wa  polisi wakati akiendesha harambee yake ya Injili mtaa kwa Mtaa mjini Iringa.


Tukio  hilo la balozi  wa Yesu  kukamatwa na  polisi  limetokea  leo majira ya saa 8 mchana   wakati gari la mwimbaji huyo wa Injili likipita katika mitaa mbali mbali ya mji wa Iringa kueneza  injili kwa kuuza CD inayokwenda kwa  jina la Saluti .

Mbali ya  kuwa na  kibali  cha Manispaa ya  Iringa  kinachompa uhuru  wa kueneeza injili kwa watu  wote kupitia CD hiyo ya  Saluti na kibali  hicho  kupitishwa  polisi  bado  askari  polisi  walimfuata  balozi huyo wa Yesu  na kumtia nguvuni kuwa hapaswi  kueneza  injili  kwa  kupiga  kelele mitaani.

Askari  ambae  jina lake  halikuweza  kunaswa  mara moja  alifika katika gari  lenye namba  za Usajili T 364 DPD ambalo  lilikuwa   limefunga  muziki mnene  na kupeperusha  injili mtaani kiasi cha  kila mmoja  mjini hapa kuvutiwa na vionjo vya mwimbaji  huyo na  kulifuata  gari hilo  kununua CD kabla ya askari  huyo  kulipiga  pini gari   hilo eneo la  Soko  kuu Miyomboni mjini Iringa .

Baada ya  kumsimamisha mwimbaji huyo kutoendelea na uuzaji wa CD  hiyo askari  huyo alimtaka  kuonyesha kibali pamoja na kuzima  muziki na kugeuza  gari hilo kupeleka  Polisi amri  ambayo bila jeuri  balozi wa  Yesu  alitii huku akisema ndio kazi ya  kueneza  injili  hiyo ambayo kwake ameizoea .

Kwa  upande  wao  wananchi ambao  walikuwa  wakinunua CD  wameeleza  kusikitishwa na hatua ya  polisi  kuzuia  uenezaji wa injili huku  kila siku mji wa Iringa  watu  wanapita na magari  wakitangaza Ma Disco na matamasha  yenye vichocheo  vya maambukizi ya VVU huku  wakiyafumbia macho.

Mtandao   huu  ulipofuatilia  sakata   hilo  kituo  cha  polisi ulishuhudia suala  hilo  likiishia nje ya  kituo  cha polisi baada ya askari  huyo  kuyamaliza  kiume na mwimbaji huyo nje ya  kituo baada ya  kuonyesha kibali halali cha Manispaa ya Iringa na wakati  askari huyo akihoji  zaidi  juu ya kuzunguka  kila  kona likiwemo  eneo hilo la polisi kwa  kupiga muziki ghalfa Mungu alionyesha nguvu  zake  kufuatia gari  jingine  lililokuwa  likiuza  simu  huku  likipiga miziki ya duniani likipita nje ya  kituo cha  polisi  bila  kukamatwa  ndipo askari kwa kuona  hilo walimruhusu  kuendelea na kazi ya kuitangaza injili.

Akizungumza na mtandao huu mara  baada ya  kuachiwa  huru Balozi wa Yesu  alisema   kuwa  polisi walifika  na kumsimamisha na kumwomba  kibali na baada ya  kuonyesha aliachiwa  huru na  kuwa  polisi  wametimiza  wajibu  wao na kuwa hana kinyongo nao.

Pia  alisema  kuwa ziara  yake  mkoani Iringa na mikoa mbali mbali ni kuitangaza  injili  kupitia oparesheni yake ya Injili mtaa  kwa Mtaa  kwa  watu  wote  waokoke  na kuwa anaifanya  hivyo kama  njia  ya kuuza CD  yake  baada ya  kuchoshwa na unyonyaji  unaofanywa na baadhi ya studio kwa kuwalalia  waimbaji wa nyimbo  za Injili nchini.
Akari  polisi  Iringa akimthibiti mwimbaji  wa nyimbo za injili mwinjilisti Joseph Nyuki maarufu kama balozi wa  Yesu  ambaye  alikuwa akiuza  CD zake  mitaani  leo

Balozi  wa Yesu  akiendelea  kudhibitiwa na polisi

Askari  polisi  akimthibiti balozi wa Yesu

Balozi wa  Yesu  akithibitiwa wakati wa kampeni yake ya Injili
Mtaa kwa Mtaa mjini Iringa  leo

Wananchi  Iringa  wakiwa  wamelizunguka gari  la Balozi wa Yesu  leo

Balozi  wa Yesu  akiwatuliza  wafuasi wake

Balozi wa Yesu  akienda  kupanda gari

Balozi  wa Yesu akiwa katika gari lake  tayari
 kwenda Polisi  kutii  sheria bila Shuluti

Gari la  balozi wa Yesu  likiondoka kwenda  Polisi

Balozi  wa Yesu  akizungumza  baada ya  kuachiwa na  polisi

Hii  ndio  CD  ya Saluti ambayo  leo balozi  wa Yesu
kajikuta  akiwapiga  kikweli kweli  Saluti  Polisi Iringa