Watu 37 wamejeruhiwa kati yao vibaya,Baada ya Basi la Kampuni ya Happy Nation lililokuwa linatoka Mbeya kwenda Dar es Salaam kuacha njia kupinduka Katika eneo la Igurusi wilaya Mbarali baada ya kupasuka tairi la Mbele na hivyo kupoteza mwelekeo na Kupinduka.
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi amesema ajali hiyo imechangiwa haswa na Mwendo kasi wa Gari hiyo licha ya jeshi la polisi kupiga kelele juu Madereva wa vyombo vya Moto kuendesha Mwendo wa Pole Kunusuru Maisha ya watu wasio na Hatia lakini Bado suala hilo linaonekana kuendelea.
Amesema baada ya ajali Majeruhi walikimbizwa Katika Hospitali ya Misheni ya Chimala kwa ajili ya kupatiwa huduma ya kwanza ambapo majeruhi kumi wamelazwa huku wa nne wakiwa wamekimbizwa hospitali ya rufaa Mbeya kwa matibabu kutokana na Hali zao zilivyo.
Aidha kwa upande wake Mganga mkuu wa hospitali ya chimala Mahenge Amesema Kuwa wamepokea majeruhi wa ajali hiyo ambapo wengine hali zao simbaya licha ya kwamba wanakabiliwa na upungufu wa Damu na wameomba msaada katika kitengo cha Benki ya Damu salama Mbeya ili kuweza kunusuru Maisha ya Majeruhi Hao.
Pia Jeshi la polisi limesema kuwa Dreva wa Gari Hilo amekimbia kwahyo linafanya Juhudi za kumtafuta ili kuweza kueleza nini sababu za ajali,ingawaje nao Abiria wamekiri kuwa Ajali hiyo ni kutokana na mwendo Kasi Uliokuwa ukisababishwa na kufukuzana na magari mengine kwajili ya Kuwahi na ndipo Likapasuka gurudumu na kuacha njia na kupinduka.

No comments:
Post a Comment