WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano Kimataifa, Mhe. Bernard Membe amekanusha bungeni taarifa za maafisa wa China kuhusika kununua pembe za ndovu wakati wa ziara ya rais wa China na kusema taarifa hizo ni za uongo na za kupika.
Waziri Membe amesema taarifa za EIA kwamba Tanzania haishughulikii tatizo la biashara haramu ya pembe za ndovu zina ajenda ya siri na mtu aliyehojiwa kama chanzo cha habari si mtumishi wa serikali, bali ni mpita njia ambaye hajui chochote
“Ziara ya Rais wa China ilichukua masaa 24 pekee, sasa hayo yote yalifanyika saa ngapi? Na kwanini taarifa hizi zitoke sasa baada ya Rais wetu kutoka nchini China na kuelezea mafanikio tuliyofikia kutokana na China”? amehoji Waziri Membe
“Kinachowasumbua hawa ni WIVU, hawataki tuendelee kama walivyoendelea wao, tuwapuuze, wanaonea wivu maendeleo ya China na ya kwetu” Waziri Membe amemaliza hotuba yake kukanusha na kulaani habari zilitotolewa na baadhi ya vyombo vya habari vya kimataifa.
No comments:
Post a Comment