Serikali imekanusha vikali habari zilizoandikwa na kutangwaza kwenye vyombo mbalimbali vya habari vya kitaifa na kimataifa na baadhi ya mitandao ya kijamii kuwa baada ya ziara ya rais wa China aliyoifanya hapa nchini mwanzoni mwa mwaka huu ndege yake iliondoka ikiwa na shehena ya meno ya Tembo.
Kauli hiyo ya seriakli imetolewa jijini Arusha na waziri wa maliasili na utalii Lazaro Nyalandu mara baada ya kufungua mkutano wa kikanda unaozungumzia njia za kukabiliana na mauaji na kuwalinda Tembo na wanyama wengine wakubwa.
Waziri Nyalandu anasema zipo baadhi ya taarifa zilizopokelewa na serikali ambazo zinafanyiwa kazi lakini anaongeza kuwa habari hizo zilizotoelwa zinalenga kuharibu uhusiano wa muda mrefu baina ya Tanzania na China.
Akizungumzia tatizo la mauaji ya Tembo nchini na nchi nyingine za Afrika na usafirishaji wa bidhaa zake afisa mtendaji mkuu wa shirika la hifadhi ya wanyamapori Afrika Dakta Patrick Bergin anasema suluhisho pekee ni kuweka sheria kali zitakazowawajibisha wahusika, hatua ambayo mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya maliasili, ardhi na mazingira mheshimiwa James Lembeli anasema itabidi sheria ya Tanzania kufanyiwa mabadiliko.
Kwa upande wake waziri kivuli wa maliasili na utalii mchungaji Peter Msigwa akaitaka serikali kutekeleza kile ilichoahidi wakati wa mkutanoni uliofanyika London Uingereza mwezi februari mwaka huu, ahadi amabazo waziri Nyalandu anasema zimeshaanza kufanyiwa kazi.
No comments:
Post a Comment