TTCL

EQUITY

Tuesday, November 25, 2014

MENGI; FURSA YA KUJIAJIRI KWA VIJANA NI MOJA YA SULUHISHO PEKEE LA TATIZO LA AJIRA TANZANIA


Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dr Reginald Mengi amesema kujiajiri ni miongoni mwa dawa za kumaliza tatizo la ajira kwa vijana kwa vile Serikali na sekta binafsi haina uwezo wa kuajiri vijana wote wanaohitimu vyuoni kila mwaka nchini.

Mwenyekiti Mtendaji wa  IPP, Dk Reginald Mengi ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati akikabidhi  ruzuku ya shilingi milioni 10  kwa mshindi wa kwanza kwa Mwezi Januari , Bw. Frederick Shayo, wa shindano la wazo la biashara analoliendesha kupitia twita yake kwa mwezi Januari.
Akikabidhi zawadi hiyo Dr Mengi amewataka vijana na wananchi kubadili fikra na kuamini kuwa kwa kutumia fursa  na raslimali za taifa wanaweza kubuni mawazo bora ya kufanya ujasiriamali utakaowawezesha kujikwamua kiuchumi na kusisitiza kuwapuuza watu  wanaodai kuwa Tanzania haihitaji mamilionea.
Dr Mengi pia amewazawadia  shilingi milioni moja kila mmoja washiriki tisa   waliofanikiwa kuingia kumi bora. Washindi hao ni  Jesse Temba, Charles Kapondo, Gerald Nyaisssa, George Rashid, na Otaigo Elisha. Wengine ni  Alphonce Mallya, Japhet Bachu, Kibanga Omari, na Emmanuel Buberwa.
Wazo la mshindi wa kwanza lilikuwa kukarabati majokofu mabovu kuyageuza kuwa viatamishi rahisi vinavyotumia umeme mdogo kwa ajili ya wafugaji wa kuku.
Mkuu wa Jopo la majaji wa shindano hilo Dr Donath Olomi ambaye ni  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Uongozi na Ujasiriamali - IMED, na majaji wenzake Bi. Ibra Maida ambaye ni  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya  IBRA Contractors, na Dr Jabu Mwasha ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tan Veterina ltd , wamesema jumla ya twiti 1,680 zilipokelewa na kushindanishwa, na kusistiza kwamba  kwa kujiamini kuwa wanaweza wameweza kumeweza kupiga hatua kubwa kwa kujiajiri wenyewe.