TTCL

EQUITY

Tuesday, November 25, 2014

Mahakama kuu yazuia mjadala wa ripoti ya akaunti ya Tegeta Escrow.

Jopo la majaji watatu wa mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam chini ya jaji Radhia Sheikhe limezuia mjadala wa ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa serikali kuhusu akaunti ya Tegeta Escrow hadi hapo hoja ya msingi ambayo ipo mahakamani itakapofanyiwa kazi.
Jopo hilo lililokuwa likiongozwa na Mh Radhia Sheikhe wameagiza kutofanyika kwa mjadala wotote kuhusu ripoti ya CAG huko bungeni na kuongeza kuwa majadiliano hayo yanaweza kufanyika baada ya shauri la msingi kupatiwa ufumbuzi.
 
Awali akizungumza na ITV mwanasheria wa IPTLl wakili Joseph Makandege amesema wamefikisha shauri hilo namba 50 katika mahakama hiyo wakitaka vifanyike vitu viwili kwanza kupata tafsiri sahihi ya kisheria kuwa kama kitendo kilichofanywana ofisi ya CAG kufanya ukaguzi katika akaunt za Escrow kama ni sahihi akaongeza kuwa wao wanachoamini ni kuwa kwa sababu jambo hilo lilikuwa limekwisha amuliwa kisheria mahakama na kwa kutolewa kwa hukumu kulikuwa hakuna haja tena na bunge kuagiza uchunguzi ufantike.
 
Aidha mwanasheria huyo akaongeza kuwa siyo kwamba hawataki jambo hilo kujadiliwa bali wanataka taratibu zifuatwe ili kuweza kufiki mwafaka wa kina katika jambo hilo mwanaasheria huyo akaongeza kuwa mbali na kupata tafsiri hiyo ya kisheria pia wanaiomba mahakama kulitaka bunge kusitisha mpango wake wakujadili tarifa ya CAG  hadi tafsiri ya kina ipatikane.
 
Mwanasheria huyo pia akasema kuwa wao wanaona kama likijadiliwa haki haitaweza kutendeka kwa sababu wao kama IPTL hawana mwakilishi bungeni na hivyo maamuzi yatafanyika upande mmoja.
 
Kwa upande wa jopo la wanasheria wa serikali wakiongozwana Obadia Kaimela wameiomba Mahakama kuwapa muda wa kuweza kuwasiliana na baadhi ya watu ama taasisi zinazohusishwa na jambo hilo ili kuweza kupata muda wa kutosha kutoa utetezi wao.
 
Kutakana na hali hiyo imeamuliwa kuwa bada ya kukamilika kwa taribu zote kesi ya msingi ikiwemo uwasilishwaji wa viapo kesi ya msingi itanza kusikilizwa Desemba 2 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment