TTCL

EQUITY

Tuesday, November 25, 2014

Umesikia hii ya Wabunge kujengewa kijiji kimoja kwa sababu ya usalama? Nimekuwekea hapa.

it_photo_90094
Katika kipindi cha maswali na majibu leo Novemba 24, Mbunge Rajabu Mbarouk Mohammed aliuliza swali; “..Suala la usalama wa Wabunge ni pamoja na maeneo wanayofanyia kazi lakini vile vile na maeneo ambayo wanayoishi wabunge, Mheshimiwa Spika tangu kuanza kwa sakata la ESCROW hali imekuwa tete kwa Usalama wa Wabunge, nini tamko la Serikali juu ya ulinzi na usalama wa Wabunge katika maeneo ya kazi lakini vile vile katika maeneo wanayoishi?..
Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Januari Makambaalijibu;”…Serikali inafanya tathimini wakati wote ya matishio ya usalama wa Nchi lakini usalama wa viongozi ikiwemo Wabunge na inachukua hatua muafaka kuhakikisha kuwa viongozi wao wako salama, kwa hiyo Serikali inapenda kuwahakikishia Wabunge kwamba licha ya yote yanayoendelea usalama wao uko salama na wasiwe na wasiwasi watimize majukumu yao kama inavyohitajika…
Naye Spika wa Bunge Anne Makinda alisema kuhusu mpango ambao Serikali inao kuhusu usalama wa Makazi ya Wabunge; “…Tunakusudia kujenga eneo la Vijiji vya Wabunge ambapo wanaweza kulindwa kwa pamoja kuliko ilivyo sasa kila kitu ni mipango…