TTCL

EQUITY

Saturday, January 4, 2014

Nini madhara ya kupenda kupita kiasi..

Female finches forced to take an inferior husband display high stress levels... just as it is in the human world

Kupenda ni jambo muhimu katika maisha ya mwanadamu, kwa sababu asilimia kubwa ya matendo ya mtu huongozwa na mapenzi. Miongoni mwetu kuna watu wanapenda
waume/wake zao, mali, watoto, magari vyakula,vinywaji, michezo na pengine aina fulani ya maisha.

Baadhi yetu tuko tayari kupoteza maisha kama tutaachwa na wapenzi au kukosa mambo tuliyoyapenda. Pamoja na kwamba moyo hupata maumivu pale mazuri yanapokosekana, bado kuna ukweli juu ya madhara ya kujitakia yanayoweza kuepukwa na mtu anayeumia kwa kiwango cha kukosa usinginzi, kulia mara kwa mara kiasi cha kushindwa kufanya kazi zake kama kawaida.

Kupenda kwa kiwango cha kushindwa kujizuia na kuvumilia ni hatari kwa afya ya mwanadamu, kwani uchunguzi unaonesha kuwa watu wengi wanaosumbuliwa na ugonjwa wa vidonda vya tumbo,moyo na wale wenye magonjwa yasiyoonekana kitalaamu pamoja na wanaokufa ghafla ni athari za msongo wa mawazo utokanao na kukosa mazuri wanayohitaji katika maisha yao.(Jiulize ni kipi kinachokutia simanzi moyoni mwako).


Kisaikolojia kuutesa moyo kwa sababu mpenzi wako kakukataa ni matokeo ya kufikiri vibaya kwani ushahidi uliopo miongoni mwetu unaonesha kuwa
mapenzi si kitu cha kudumu kwa miaka mingi na anayesema anaweza kupenda jambo moja milele kwa kiwango kilekile ni mtu anayejiwekea mtengo utakaomnasa mwenyewe na kumtesa.
Toa maoni yako…

No comments:

Post a Comment