TTCL

EQUITY

Wednesday, November 20, 2013

WACHINA WASHIKWA NA KIGANJA CHA MFANYAKAZI WAO KILICHOFUKIWA KARIBU NA ENEO LA KIWANDA!!!

WACHINA wawili wa Kiwanda cha Urafiki Plastic cha jijini Dar es Salaam wanashikiliwa na polisi wa Kituo cha Magomeni kwa tuhuma za kukutwa na kiganja cha mfanyakazi wao, Jumanne Rashid, kilichofukiwa kwenye eneo la kiwanda hicho.
 
 Mmiliki wa kiwanda hicho, Lee Sliim, akiwa ndani ya gari la Polisi kuelekea kituoni kwa mahojiano zaidi.
 
Akielezea tukio hilo kwa waandishi wa habari jana, ndugu wa Jumanne aliyejitambulisha kwa jina la 
Rehema Rashid, alisema Novemba 17 mwaka huu  majira ya saa 3:00 usiku walipata taarifa kuwa  ndugu yake alipata ajali ya kukatwa mkono  na mashine kiwandani hapo.

Alisema baada kupata ajali hiyo, Wachina hao kwa kusaidiana na wafanyakazi wengine walimpeleka katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu, ambapo ndugu wote waliendelea na huduma ya kumuuguza.
 
 Mkono wa mtu uliopatikana kandokando ya Kiwanda cha kutengeneza mifuko ya Viroba na Plastiki, Mababi jijini Dar.
 
Rehema alisema jana wakiwa katika pilikapilika za kwenda kumjulia hali ndugu yao, walipata taarifa kwa wasamaria wema kwamba kiganja cha mkono wa ndugu yao kimeonekana kikiwa kimefukiwa pembezoni mwa kiwanda hicho.

“Leo asubuhi tukiwa katika maandalizi ya kwenda kumwona Jumanne, tulipata taarifa kutoka kwa wasamaria wema ambao wanafanya shughuli za kufua vyuma chakavu karibu na kiwanda hicho wakitutaka twende kutambua kama kiganja kilichofukiwa ni chake,” alisema Rehema

No comments:

Post a Comment