TTCL

EQUITY

Friday, November 29, 2013

MGANGA WA KIENYEAJI AMUUA MTEJA WAKE WA KIKE BAADA YA KUVUTA UUME WAKE ALIPOTAKA KUFANYA NAYE MAPENZI.

MGANGA wa kienyeji Jumatano aliieleza Mahakama Kuu kwamba, “alimuua mwanamke wa miaka 18 kwa sababu alimvuta uume wake walipovua nguo kushiriki ngono.


Lakini Jaji Florence Muchemi alimwamuru  Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Keriako Tobiko awasilishe ushahidi katika kesi hiyo. Jaji Muchemi alimweleza Geoffrey Wanjala Wechule ushahidi utawasilishwa kortini ndipo “ korti iamue ikiwa yuko na kesi ya kujibu au la.”

Bw Wechule mwenye umri wa miaka 36 alikiri  alimuua Jane Kadogo Mutiso siku kuu ya Mashujaa Oktoba 20 katika eneo la Gitina mtaani Kawangware Kaunti ya Nairobi.

Tangu afikishwe kortini Oktoba 22 mshtakiwa amedumisha  kusema kwamba alimuua Kadogo na yuko “tayari kufa.”

Aliposomewa shtaka Jaji Muchemi alimwuliza , “Unasemaje kuhusu shtaka inayokukabili. Ulimuua Jane Kadogo Mutiso au hakumuua?”

“Nilimuua  Kadogo. Nilikuwa na sababu ya kumuaa,” Bw Wechule akajibu.

“Ulimuua kwa sababu gani,” Jaji Muchemi alimtaka aeleze.

“Nilimuua kwa sababu alifuruta uume wangu. Alinifuta sehemu zangu nyeti,” mshtakiwa alimjibu Jaji Muchemi.

“Hii korti imechukulia kwamba umekana shtaka. Nimeandika kwamba umekana shtaka ijapokuwa unakiri. Lazima DPP awasilishe ushahidi ndipo uamuzi utolewe,” Jaji Muchemi alimweleza mshtakiwa.

Mahakama iliamuru Kesi hiyo itajwe Desemba  9, 2013 maagizo zaidi yatolewe.

Jaji Muchemi aliamuru mshtakiwa azuiliwe katika gereza la Viwandani hadi siku hiyo.

Mahakama iliamuru kiongozi wa mashtaka Daniel Karuri amkabidhi mshtakiwa nakala za kesi ndipo aandae tetezi zake.

Bw Wechule anadaiwa alimuua Kadogo alipokataa kushiriki mapenzi naye siku kuu ya mashujaa licha ya kwamba walikuwa wamesikizana na hata walikuwa wamevua nguo wakabaki uchi wa mnyama. Kisanga hicho kilitendeka katika eneo la Gatina, Mtaa wa Kawangware, Kaunti ya Nairobi. Mshtakiwa alikuwa mkakamavu alipokuwa anajibu kwamba alimuua Kadogo.

No comments:

Post a Comment