TTCL

EQUITY

Saturday, November 16, 2013

BODABODA AJIRA LAKINI BOMU LAKULIPUA MAISHA YA WENGI, ULEMAVU NA VIFO NDIO KHARARAHAA...

Maskini! Dereva wa pikipiki ya abiria maarufu kama bodaboda jina halikunaswa mara moja kwa kuwa alikuwa hawezi kuzungumza amepata ajali mbaya na kuvunjika mguu wa kulia kisha kukatika vidole vitatu vya mkono wa kulia.



Muonekano wa pikipikibaada ya ajali.
 
Tukio hilo lilitokea juzi mara baada ya jamaa huyo kugongwa na lori la mchanga katika eneo la Daraja la Mkolani wilayani Nyamagana nje kidogo ya Jiji la Mwanza.



Amepata ajali mbaya na kuvunjika mguu wa kulia kisha kukatika vidole vitatu vya mkono wa kulia.
 
Kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwa eneo la tukio, baada ya jamaa huyo kuumia vibaya, wasamaria wema walijitokeza na kumkimbiza kwenye Hospitali ya Rufaa ya Bugando.
Habari zilieleza kuwa dereva huyo alikuwa akitokea maeneo ya Mkolani kuelekea Buhongwa ambapo lori lililomgonga lilikuwa Buhongwa kuelekea Mkolani.
Ilidaiwa kuwa dereva wa lori ‘aliovateki’ daladala iliyokuwa mbele yake na baada ya kuipita ndipo akakutana uso kwa uso na bodaboda.

No comments:

Post a Comment