TTCL

EQUITY

Saturday, August 24, 2013

Kwa mfano dingi kazingua, utakisanua?


 
Kuna dogo jana pale Tabora alikuja kunizingua kinomanoma, sijui alitumwa yule au ndiyo kaamua tu kwamba kinuke yaishe? Ujue hawa madogo samtaimz msiwalete kwenye hizi bata, tutawaumiza.
Unajua ilikuwaje?
Dogo kaja anataka kujua kama andagraundi wataruhusiwa kupafomu ama nini? Mimi siyo sekta yangu nikamwambia mstue dazeni ndiyo ishu zake hizo mimi mtu wa `nyuzpepaz’.
Kanigomea kudadadeki zake, haukamz? Mi wewe ndiyo nakujua kwa hiyo kama vipi we nenda kamstue, mi nakungoja hapa unipe jibu.
Nikamuuliza kwa hiyo dogo unanituma?
Dogo unafikiri kajibu? Akanikunjia uso akawa ananicheki tu. Sasa mi si unanijua mtu mzima? Nikashtukia tu kwamba hizi ni `rizati’ za ganja za utotoni, unajua ganja nazo bwana ukizianza mapema unaweza ukamzingua hata dingi yako, mi nikajifanya kama naenda kumshtua dazen, nikaishia huko huko sikurudi.
Enewei tulikuwa Tabora kwenye Fiesta na leo nimelikita ukweni unaambiwa. Kila demu ninayemsalimia ananiita shemeji, najiuliza haukamz kudadadeki?
Eneweiz mashemeji mziki upo kesho, karibuni uwanjani chama kubwa Mwanaspoti linakuja kukamua ndani ya Fiesta, mnanisoma?
sasa leo nataka tudiskasi mambo ya adabu kidogo sababu mwanangu mwenyewe Kandoro yamemkuta rodini huko kwenye mitikasi yake, na haya mambo ya mjini ...kikanuka ile ile kudadadeki.
Uliza ilikuwaje?
Mwana alikuwa anakula ndefu, mitaa ya baga nini akaskilizie upepo wa baharini, si unajua zile? Basi mwanangu katika kukamua nini barabarani si likaibuka daladala, likawa kama linataka kumchomekea, akaona ujinga, akamkazia. Kumkazia na mwenye daladala naye akawa kama anakaza hivi, kha ...kikalia mwanangu kizinga.
Halafu mwanangu alikuwa anasukuma kitu cha mjerumani, kikawa kama kimeparuzwa upande mzima hivi, ikabidi, Kandoro ashuke, akaenda kuchomoa funguo za daladala, akaenda mbele ya gari lake, akawa kalikita anasubiri mwafaka wa nini kije kufuata baada ya ajali.
Uliza nini sasa?
Alishuka mshua huyo kaenda eji kuliko matarajio unaambiwa, fulu mvi kichwani unaambiwa akamuendea Kandoro, akaanza kumletea za kiutu uzima zile za “...hujambo mwanangu?”.
Kandoro nguvu kama zikamwishia hivi unaambiwa, kabla hajamjibu unaambiwa dingi akajitupa chini akaanza kumshika miguu Kandoro, anamwomba msamaha, hadithi kibao unaambiwa zikaanza kum’mwagika.
Unaambiwa mzee akaanza kuleta zile za “...mwanangu, unajua siyo mimi, wadogo zako nyumbani ndiyo wanayataka haya, kama wangesoma mimi saa hizi ningekuwa nimepumzika, lakini inabidi babaako nihangaike na dunia, nakuomba radhi mwanangu nisamehe niko chini ya miguu yako”.
Mshua alipoona Kandoro haoneshi kujali akaanza kuangusha na chozi yaishe, unaambiwa kalia kama mtoto mdogo mpaka kila mtu akawa anamwonea huruma.
Ilibidi Kandoro amteme yule dingi aende zake lakini ndiyo akawa kashakula losi ya maana kutokana na mazingulizi ya mshua. Mi nilikuwa pembeni hapo nashuhudia muvi zima nikajiuliza ina maana huyu mshua alipokuwa anakaza alikuwa hakumbuki kama kuna watoto homu?
Au ndiyo kwa sababu alikuwa anasukuma daladala, akawekeza na akili zake kidaladala?
Mimi kama zee nawaambia washua wote ambao wana hizi ishu za kujitoa akili wanapokuwa katika mitikasi ya town kwamba siku wakiingia katika kumi na mbili zangu...
Tutaelewana hakyanani.
Singida, kesho basi uwanjani pale tukaone itakuwaje au siyo?
Pamoja!

No comments:

Post a Comment