Ngege maalumu ya Rais Tanzania pia hutumika kubeba viongozi wa Serikali.
WABUNGE wa CCM Zanzibar wameibua
zengwe jipya dhidi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad kwamba
anatumia ndege ya Rais kubebea mkaa, mihogo na ndizi kutoka Pemba
kwenda Unguja.
Habari
zilizopatikana kutoka ndani ya serikali ya Mapinduzi Zanzibar zinaeleza kuwa,
tuh
uma hizo zilitolewa na wabunge hao wakati wa kikao chao na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein mwezi uliopita.
uma hizo zilitolewa na wabunge hao wakati wa kikao chao na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein mwezi uliopita.
Kitendo hicho kinachodaiwa kufanyika
mwezi uliopita kimeonekena kuwakera baadhi ya viongozi wa Serikali wakiwamo
wabunge wa CCM Zanzibar, ambao wakati wa kikao hicho na Rais Dk Shein mwezi
uliopita mjini Zanzibar, walilizungumza kwa uchungu na kuomba Rais amuonye
Maalim Seif kwa kuigeuza ndege ya Rais kuwa ya mizigo.
Anayedaiwa kuibua hoja hiyo ni
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Taifa (UVCCM), Sadifa Juma Khamis, ambaye alisema
kuwa kitendo hicho cha Makamu wa Kwanza wa Rais kutumia ndege hiyo kubebea
mkaa, mihogo na mikungu ya ndizi kinadhalilisha Ofisi ya Rais.
Katibu wa Wabunge wa CCM Zanzibar,
Mbunge wa Magomeni, Mohammed Chombo alipoulizwa na gazeti hili kuhusiana na
suala hilo alikiri wabunge hao kulifikisha suala hilo kwa Rais Shein.
“Tulimweleza Rais matatizo mengi
likiwamo na hilo la Makamu wa Kwanza wa Rais kutumia ndege ya Serikali kubebea
mihogo na mkaa,” alisema.
Alisema kuwa Rais aliwaambia kuwa
ameyapokea malalamiko hayo na kwamba atayafanyia kazi.
Chombo alisema kuwa kwa sasa
wanamsubiri Rais Shein awaite kuwapa majibu ya matatizo yao.
Baadhi ya wabunge wa CCM Zanzibar
ambao walizungumza na gazeti hili, walisema kuwa kitendo hicho ni matumizi
mabaya ya mali za umma kwa sababu kuna vyombo vingi vya usafiri vinavyoweza
kutumika kusafirishia mizigo hiyo.
Ofisa mmoja ambaye hakutaka kutajwa
jina lake kutoka Mamlaka ya Ndege za Serikali, akizungumzia utaratibu wa
viongozi wa Serikali kutumia ndege hizo, alisema viongozi wa juu wa Serikali ya
Muungano na Zanzibar hukodi ndege zao.
Alisema hajawahi kuona ndege kubebea
mkaa, hata ndege ya jeshi hajawahi kuona ikibeba mkaa.
Hata hivyo, Katibu wa Wabunge wa
CUF, Mohammed Habibu Mnyaa, alisema madai hayo ya wabunge wa CCM ni siasa chafu
dhidi ya Makamu wa Kwanza wa Rais na kwamba wao wanaamini hawezi kufanya jambo
hilo. MWANANCHI
No comments:
Post a Comment