TTCL

EQUITY

Saturday, August 24, 2013

Changamoto za vijana wa zama hizi

Kidele alimnunulia mtoto wake wa miaka 6 hivi kigari cha kuchezea chenye muundo wa basi. Siku moja wakati Kidele yupo jikoni mwanae alikuwa sebuleni anachezea kile kigari. Kidele akawa anamsikiliza mtoto wake wakati anaongea na kigari na vitoi vyake vingine.

Mtoto akatoa sauti kama ya gari linavyofanya kisha akapiga breki na kusema “Haya mwisho wa gari sishobokei abiria wa mtu toeni makalio yenu katika siti muende makwenu. Na nyinyi mlio kituoni kama mna safari ingizeni makalio yenu katika siti haraka tunawahi mingo sasa hivi. Kama unajijua we ni denti nisikute makalio yako katika kiti nitakupasua bichwa lako”

Kidele aliposikia maneno hayo toka kwa mtoto wake akaenda sebuleni kwa hasira na kumsema mtoto wake “Lugha gani hiyo chafu unayotumia humu ndani, nisikusikie tena. Nenda chumbani kwenu ukakae bila kucheza kwa muda wa masaa mawili kama adhabu yako.”

Mtoto wake akaenda chumbani huku anatia huruma na kutumikia adhabu yake ya masaa mawili bila ya kucheza. Baadae akatoka na kuendelea kucheza. Kidele alikuwa bado yupo jikoni akamsikia mtoto wake akicheza tena na kuanza kama mwanzo.

Yule mtoto alipofunga breki ya kigari chake akaanza tena “Wapendwa abiria wetu tunashukuru kwa kuchagua gari letu, Huu ndio mwisho wetu wa safari na tunatumai mmefurahia huduma yetu, karibuni sana.

Haya mlio kituoni karibuni sana katika gari letu ndio linaanza safari ya kuelekea mjini, safirini nasi kwa safari ya utulivu na salama”

Kidele alipokuwa anasikia maneno haya akafurahi sana kuona mwanae amejeirekebisha, akaanza kutabasamu wakati mtoto anaendelea kuongea, mtoto akaendelea kumalizia kuongea na abiria wanaotaka kupanda gari “Na kama kuna abiria yeyote aliyesubiri kituoni kwa masaa mawili yaliyopita na amekasirishwa na kitendo hicho aende akapeleke malalamiko yake jikoni kuna jitu limeweka makalio yake katika kigoda kazi yake kunisikiliza na kunipa kifungo ninapokosea”

No comments:

Post a Comment