TTCL

EQUITY

Thursday, July 4, 2013

SHILOLE!!

Eti, Hata uwe “pedeshzee” wa aina gani, bila mambo “flani” hupati kitu kwa Shilole!

Eti, Hata uwe “pedeshzee” wa aina gani, bila mambo “flani” hupati kitu kwa Shilole!

Mwigizaji na mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Zena Mohamed, maarufu kama shilole amedai kuwa anaweza kufanya ujinga wowote humu duniani lakini linapokuja suala la mapenzi kamwe hawezi kwenda bila kutumia zana ama pekupeku kama watoto wa mjini wanavyosema kwani anaogopa sana gonjwa hili lisilotibika la UKIMWI ambalo limewamaliza mastaa kadhaa nchini na bado linaendelea kuwatafuna wengi waliosalia.
Akiongea alisema kuwa hata mtu awe vipi, au awe wa dini gani au awe na pesa kiasi gani kamwe hawezi kumkubalia kufanya naye kitendo hicho kilichokatazwa kabla ya ndoa bila kutumia kinga na alizilaani kauli zinasema eti ukitumia kinga ladha ya mapenzi inapungua kuwa si za kweli na za kijinga.
“Unajua nini mwandishi, najipenda na nayapenda maisha yangu, mimi ni mrembo, nisipojilinda nani atanilinda?” Aliongeza Shilole Hata niwe nimelewa kiasi gani huwa nipo makini sana maana najua vijana wengi wa mjini wananimendea sana” Alizidi kusisitiza mrembo huyo.

No comments:

Post a Comment