TTCL

EQUITY

Friday, July 5, 2013

JKT YAFUNGUA MASHINDANO YA KUADHIMISHA MIAKA 50

Mkuu wa JKT Meja Jenerali Raphael Muhunga akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa michezo ya kusherehekea miaka 50 ya JKT iliyoanza leo katika viwanja vya Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam
 
 Baadhi ya wachezaji wakipita kwa maandamano mbele ya mgeni rasmi wakati wa uzinduzi wa michezo ya kusherehekea miaka 50 ya JKT.
 
 Macho mbeleee.
 
 Mkuu wa JKT Meja Jenerali Raphael Muhunga akisalimiana na wachezaji wa timu ya Kanembwa JKT ya Kigoma.

Mkuu wa JKT Meja Jenerali Raphael Muhunga akisalimiana na wachezaji wa JKT Ruvu kabla ya mpambano wao na Kanembwa JKT.
 
 Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu zote mbili.

Na Mwandishi wetu

JESHI la Kujenga Taifa (JKT), limezindua michezo mbalimbali kuelekea maadhimisho ya  kusherehekea miaka 50 tangu kuanzishwa kwake.

Michezo hiyo imezinduliwa leo katika uwanja wa Karume na maadhimisho yake yatafanyika Julai 10 katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Meja Jenerali Raphael Muhunga ambaye ndio alikua mgeni rasmi katika uzinduzi huo aliwataka wanamichezo kufanya vizuri katika mashindano hayo ambapo kutakua na zawadi kwa washindi siku ya kilele cha maadhimisho hayo.

Alisema lengo la mashindano hayo ni kuadhimisha miaka 50 ya JKT ambayo yataenda sambamba na maonesho mbalimbali ambayo pia yatazinduliwa rasmi leo katika kikosi cha 831 Mgulani JKT.

Alisema timu nne za JKT ambazo zinashiriki ligi kuu Tanzania Bara, Ruvu Shooting, Mgambo Shooting, JKT Oljoro na JKT Ruvu zitakua zinaiwakilisha JKT ikiwa ni pamoja na timu ambazo zinacheza ligi daraja la kwanza Tanzania bara, Kanembwa JKT ya Kigoma na Mlale JKT ya Ruvuma.

“Tunategemea kwa hapo baadae, JKT kupitia kurugenzi ya Elimu na Michezo inatakiwa kuwa na shule ya kukuza vipaji vya wanamichezo kama zinavyofanya nchi za wenzetu, tunaamini kwa kufanya hivi michezoitakua hapa nchini.

Alisema JKT wanaendelea kuwatumia vijana wanaojiunga na mafunzo ya JKT ili kupata achezaji bora watakaoliwakilisha Taifa letu katika michezo mbalimbali ya Kimataifa.

No comments:

Post a Comment