NJIA KWA VIJANA KUCHEZA SOKA ULAYA YAANZISHWA!!
>>KAMPUNI YA MWANDI YAANDAA MICHUANO, MAFUNZO DAR!!
>>LIPA LAKI 3, UPATE FURSA KUCHEZA PROFESHENALI ULAYA NA DUNIANI KOTE!!
PATA TAARIFA KAMILI:
KAMPUNI YA TANZANIA MWANDI YAANZISHA MICHUANO YA AFRICAN YOUTH FOOTBALL TOURNAMENT
Kampuni ya Tanzania Mwandi kwa kutambua
kuwa Tanzania na Afrika nzima kuna vijana wengi ambao wana vipaji vya
mpira wa miguu na hivyo wanachohitaji ni kuonyeshwa tu jinsi ya kuufikia
‘Ulimwengu Halisi’ wa Mpira duniani Tanzania Mwandi imeamua kuanzisha
michuano ya African Youth Football Tournament ambayo itawashirikisha vijana wenye umri kati ya miaka 18 hadi 21.
Michuano hiyo itaambatana na mafunzo kwa
siku tano ambapo vijana hao watapata mafunzo ya mpira wa Miguu (elimu,
ujuzi na hata mbinu za uwanjani) kutoka kwa makocha wawili wa hapa
nchini na watatu wa kimataifa kutoka nje ya nchi, kuanzia tarehe
10/06/2013 hadi tarehe 14/06/2013 katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.
Aidha, mafunzo yatafanyika nyakati za
asubuhi na jioni wachezaji hao watashiriki Mashindano ya kucheza wao kwa
wao ili kupata vijana 11 bora miongoni mwa wachezaji watakaoshiriki.
Wachezaji Bora 11 watakaopatikana watakuwa mabalozi wa Mdhamini Mkuu wa Michuano ya African Youth Football Tournament
na watapata fursa ya kutangazwa zaidi kimataifa na kutafutiwa vilabu
vya kucheza soka Barani Ulaya katika nchi nane (Ufaransa, Ureno, Uswis,
Ubelgiji, Uholanzi, Norway, Sweden na Denmark pamoja na barani Afrika na
Asia.
Ili kupanua wigo wa kuwatangaza
kimataifa wachezaji wengi zaidi, Michuano hii pia itaalika skauti na
mawakala wa soka wa kimataifa ili kufuatilia uwezo wa wachezaji hao
asubuhi katika mazoezi na jioni kwenye michuano, kuwapata vijana bora
ambao watapendelea kuwatafutia timu nje ya nchi kukipiga huko kwa
makubaliano ambayo pande hizo mbili (mchezaji na wakala) zitaafikiana.
Miongoni mwa Mawakala ambao watakuwepo
ni wakala wa Kimataifa wa Tanzania, Dk. Damas Ndumbaro, Phillip
Mwakikosa (Sweden) na wengine wengi.
Hata hivyo kutokana na gharama kubwa za
uandaaji wa Michuano hii, na ndio kwanza ikiwa inaanzishwa, Kampuni ya
Tanzania Mwandi kwa kujali mahitaji ya Kitanzania tumeweka kiingilio kwa
mchezaji wa Tanzania kuwa shilingi laki tatu (Tsh. 300, 000) na
mchezaji wa nje ya Tanzania Dola 500 za Kimarekani (USD 500).
Fedha hizo zitagharamia malazi, chakula na mahitaji mengine yote kwa mchezaji pindi atakapokuwa kambini.
Hii ni fursa adimu kwa vijana wa
Kitanzania kuonyesha uwezo wao ili kutimiza ndoto za kucheza soka barani
Ulaya, Asia na barani Afrika katika vilabu vikubwa huku ikikumbukwa
kuwa mnamo Mwaka 2012 ni wachezaji wachache sana wa Kitanzania waliopata
fursa ya kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa kutokana na
uchache wa mawakala na gharama hivyo kuletwa mawakala hao nyumbani
Tanzania ni fursa pekee ya kufikia malengo.
Mpaka sasa tayari Kampuni ina majina
takribani ya vijana 10 wa Nje ya nchi (Uganda, Nigeria na Ghana) ambao
wameomba kushiriki hivyo tunatoa wito kwa Watanzania kutoipoteza fursa
ya kuletewa njia ya kuelekea kusakata soka Barani Ulaya mlangoni mwao.
Lakini tunafahamu hali halisi ya maisha
yetu kwahiyo nitoe wito kwa Wadhamini mbalimbali ambao tumewaomba
kutusaidia kufanikisha Mashindano haya ambayo naamini yatalitangaza
taifa letu na kulitangaza zaidi soka letu kimataifa. Pia udhamini wao
utatuwezesha kupunguza hizi gharama kwa washiriki kutoka Tanzania na
hivyo kuwachukua vijana wengi zaidi.
Kampuni ya Tanzania Mwandi ni Kampuni
binafsi ambayo imejikita katika kuendeleza sekta za utalii, michezo na
burudani ndani na nje ya nchi na hivyo kuiongezea kipato nchi moja kwa
moja ama kupitia kuwawezesha wananchi kama vile kuwatengenezea fursa za
ajira vijana kupitia michezo.
Fomu za ushiriki Michuano hii zinapatikana kupitia www.tanzaniamwandi.co.tz na www.blog.tanzaniamwandi.co.tz
“African Youth Football Tournament; Live your Dream.”
No comments:
Post a Comment