TTCL

EQUITY

Friday, February 19, 2016

Wadau wa sukari wanena kauli ya Rais Magufuli

Wadau wa sukari nchini Tanzania wamepongeza hatua ya Rais Magufuli kuhusu uingizwaji vibali huku wakiiomba kushughulikia zaidi na njia za magendo ambazo hutumika kuingiza sukari hiyo ikiwa ni pamoja na kuteketeza sukari inayokamatwa.
 
Sukari ikiwa imehafadhiwa kwenye ghala la sukari kwenye moja ya viwanda nchini. 
 
Ofisa Mtendaji Utawala wa Kiwanda cha Sukari TPC, Mkoani Kilimanjaro, Jaffary Ally amesema kwa miaka mitatu viwanda vya ndani vimekandamizwa na sukari ya magendo ambayo huuzwa kwa bei rahisi na kuwalazimu wazalishaji wa ndani kuuza kwa bei ya chini ya uzalishaji
Bw. Ally amesema Sukari hiyo kutoka nje iliathri mtiririko wa fedha, bei ya miwa inayonunuliwa kutoka kwa wakulima na nje ya viwanda vya Kilombero na Mtibwa, uwezo wa viwanda kulipa mikopo ya benki, wasambazaji, kuongeza mishahara na marupurupu ya wafanyakazi
Ofisa huyo ameongeza kuwa uamuzi wa Rais utalinda na kuimarisha viwanda vya ndani na walaji kwa kuwa sukari ya nje iliingia bila kupimwa na hivyo kuathiri watumiaji na viwanda vya kuzalishia sukari.
Amesema kuwa kwa sukari ya magendo inayoingizwa nchini kila mwaka inaikosesha serikali kodi ya karibu dola milioni 40 (sawa na Tsh. bilioni 87) fedha ambazo zingeokolewa zingesaidia kunyanyua maendeleo ya nchi kwa kiasi kikubwa.
Kwa upande wake Kaimu Mneja Uzalishaji wa Kiwanda cha Sukari cha Mtibwa kilichopo Mkoani Morogoro, Hamad Yahaya amesema pamoja na hatua njema ya Rais lakini lazima alinde mipaka ambayo ina njia nyingi za panya zinazotumika kuingiza sukari nchini.

No comments:

Post a Comment