>>XAVI NJE, MESSI KUCHEZA LICHA YA HOMA!!
>>MOURINHO KUPANGUA KIKOSI, KUIVIZIA MAN UNITED!!
NDANI
YA Siku 4 baada ya Real Madrid kuichapa Barcelona Bao 3-1 Uwanjani Nou
Camp na kuwatupa nje ya COPA del Rey, leo tena Timu hizo zinakumbana
safari hii ndani ya Uwanja wa Santiago Bernabeu kwenye Mechi ya La Liga.
Real Madrid, ambao ndio Mabingwa
watetezi wa La liga, wako nafasi ya 3 kwenye Ligi hiyo inayoongozwa na
Barcelona ambao wako Pointi 16 mbele ya Real na Pointi 12 mbele ya Timu
ya Pili Atletico Madrid.
ZIFUATAZO NI DONDOO MUHIMU KUHUSU MECHI HII:
HALI ZA WACHEZAJI:
Real
Madrid inaweza ikawachezesha Marcelo, Luka Modric, Kaka na Karim
Benzema ambao wote hawakucheza waliposhinda 3-1 kwenye Copa del Rey
Jumanne huko Camp Nou.
Pia
Beki Sergio Ramos, baada ya kutumikia Kifungo cha Mechi 1, anaweza
kucheza lakini Winga Angel Di Maria hatacheza baada ya kupewa Kadi
Nyekundu walipocheza na Deportivo La Coruna.
Barcelona
huenda wakamkosa Kiungo Xavi ambae ni majeruhi na pia Nyota wao Lionel
Messi anatarajiwa licha ya majuzi kukosa mazoezi aliporitiwa anaugua
homa.
TATHMNI YA MECHI:
Mechi
ya kwanza ya La Liga Msimu huu kati ya Mahasimu hawa iliyochezwa hapo
Oktoba 7 huko Nou Camp ilimalizika kwa Bao 2-2 huku Nyota Lionel Messi
na Cristiano Ronaldo wakifunga Bao 2 kila mmoja kwa Timu zao.
Akiongelea Mechi hii, Kocha Msaidizi wa
Barcelona Jordi Roura, ambae ndie ameshika hatamu kwa kukosekana Kocha
wao Tito Vilanova ambae ni mgonjwa, amesema: “Tulipocheza na AC Milan na
Real hatukuwa na cheche zetu na hili lisituvunje moyo. Leo, Timu
itajituma na kushindana kwa kila kitu.”
Roura alikiri kuwa Wachezaji wake
wameumizwa na vipigo vya 2-0 toka kwa AC Milan na 3-1 toka kwa Real na
pia alimtetea Nyota wao Lionel Messi alieshindwa kufurukuta kwenye Mechi
hizo mbili ambazo alishindwa hata kupiga Shuti moja lililolenga Golini
na hiyo ni mara yake ya kwanza kwa kitu hicho kumtokea Msimu huu.
Kambi ya Real haijazungumza lolote
kuhusu Mechi ya leo lakini inaaminika Kocha Jose Mourinho huenda
akapangua Kikosi chake cha leo kwa vile wameshakata tamaa kutetea Taji
lao la La Liga na pia Jumanne wana Mechi ngumu ya UEFA CHAMPIONZ LIGI
huko Old Trafford dhidi ya Manchester United wanayotakiwa kuifuta sare
ya 1-1 waliyotoka na Man United katika Mechi ya kwanza.
USO kwa USO:
COPA del REY 26 Feb: Barcelona 1 Real Madrid 3
COPA del REY Jan 30: Real Madrid 1 Barcelona 1
LA LIGA Okt 7: Barcelona 2 Real Madrid 2
SUPERCOPA Ago 29: Real Madrid 2 Barcelona 1
SUPER COPA Ago 23: Barcelona 3 Real Madrid 2
DONDOO za KUMBUKUMBU:
Real Madrid
-Wameshinda Mechi zao 10 kati ya 11 zilizopita walizocheza Nyumbani na hawajafungwa katika Mechi 24 zilizopita.
-Msimu huu Real wamefunga jumla ya Mabao 101 katika Mechi zao 42 hadi sasa.
Barcelona
-Wameshinda Mechi 3 tu kati ya 7 walizocheza mwisho katika Mashindano yote na kufungwa 2 na sare 2.
-Katika Mechi 7 walizocheza mwisho na Real Madrid, Barca wameshinda Mechi 1 tu na kufungwa 3 na sare 3.
VIKOSI VINAVYOTARAJIWA KUANZA:
REAL MADRID [Mfumo: 4-2-3-1]:
Diego López
Arbeloa • Sergio Ramos • Pepe • Marcelo
M. Essien • L. Modrić
José Callejón • Kaká • Cristiano Ronaldo
K. Benzema
BARCELONA [Mfumo: 4-3-3]:
Valdés
Dani Alves • Piqué • J. Mascherano • Jordi Alba
Xavi • Busquets • Iniesta
Pedro • L. Messi • David Villa
Refa: Miguel Pérez
LA LIGA
RATIBA/MATOKEO:
Ijumaa Machi 1
Getafe 2 Real Zaragoza 0
Jumamosi Machi 2
Real Madrid CF v FC Barcelona [SAA 12 JIONI]
Deportivo La Coruna v Rayo Vallecano
Osasuna v Athletic de Bilbao
Valencia v Levante
Jumapili Machi 3
Granada CF v Real Mallorca
RCD Espanyol v Real Valladolid
Malaga CF v Atletico de Madrid
Real Sociedad v Real Betis
Jumatatu Machi 4
Sevilla FC v Celta de Vigo
No comments:
Post a Comment