Takriban raia 132
wa Tanzania wanaoishi nchini Msumbiji wamefurushwa nchini humo huku
wengine wasiojulikana wakidaiwa kukamatwa kufuatia operesheni
ilioanzishwa na serikali ya taifa hilo.
Kulingana na serikali ya Msumbiji operesheni hiyo inalenga kuwatimua raia wa kigeni wanaoishi nchini humo kinyume cha sheria.
Taarifa
ya wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki nchini
Tanzania imesema kuwa raia waliofukuzwa ama hata kukamatwa ni wale
wanaoishi mji wa Monte Puez kwa kuwa una raia wengi wa kigeni
ikilinganishwa na miji mingine.
Kulingana na taarifa hiyo tayari
ubalozi wa Tanzania nchini Msumbiji unaendelea kufanya mawasiliano ya
kidiplomasia na serikali ya Msumbiji ili kuwahakikishia usalama raia wa
Tanzania na mali yao nchini humo.
Inakadiriwa kuwa, Watanzania wapatao elfu tatu (3,000) wanaishi na kufanya shughuli za kiuchumi na kijamii katika mji huo wa Monte Puez.
Hatua hiyo inajiri licha ya mataifa ya Msumbiji na Tanzania kufanya mkutano wa kuainisha maeneo ya ushirikiano yakiwemo maswala ya kibiashara na uhamiaji.
Na huku operesheni hiyo ikiendelea serikali ya Tanzania imekuwakumbusha Watanzania wote waishio ughaibuni, kufuata Sheria na taratibu za nchi hizo wanazoishi.

No comments:
Post a Comment