Kamanda Sirro akizungumza na wanahabari leo |
Leo Februari 16, 207 Jeshi la Polisi Kanda
Maalum ya Dar es Salaam limetoa taarifa ya kukamatwa kwa jumla
watuhumiwa 349 katika oparesheni ya kuwasaka watu wanaohusika na dawa za
kulevya.
Akizungumza
leo Jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum
ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro amesema kati ya watuhumiwa hao
wamo wauzaji, wasafirishaji na watumiaji wa dawa za kulevya, na
kwamba Wataanza kufikishwa mahakamani siku ya kesho, huku mmoja
akipandishwa kizimbani leo.
Pia ametoa taarifa ya kijana mmoja anayedaiwa kusambaza taarifa za
uongo, ambapo amesema kuwa jeshi hilo linamshikilia kijana huyo ambaye
ni mwanafunzi mwenye umri wa miaka 23, anayedaiwa kutaja majina ya
viongozi na kuwatuhumu kuwa wanahusika na dawa za kulevya.
Kuhusu askari 9 waliotuhumiwa kuhusika na dawa hizo, Kamanda Sirro
amesema askari hao wamekabidhiwa kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya kuzuia
na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za
kisheria.
Kamanda Sirro amesema hadi sasa jumla ya kete 612 pamoja na bangi
vimekamatwa na kwamba kuna watu wengine 17 ambao bado jeshi hilo
linawafuatilia na watakuwa mbaroni wakati wowote.
Kijanaanayedaiwa kutaja majina feki ya vigogo watumia unga. |
No comments:
Post a Comment