Naibu Waziri, Wizara ya
Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazia Wambura (Mb) akiongea
na Wabunge wenzake (hawapo pichani) kuhusu umuhimu wa kufanya mazoezi
kwa ajili ya kulinda afya ya miili pamoja na matarajio ya Uzinduzi wa
Mazoezi yanayotarajiwa kuzinduliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania ambayo yatatangazwa hivi karibuni.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Mhe.
Ritta Kabati akiongea na Wabunge wenzake pamoja na Waandishi wa habari
kuhusu umuhimu wa kufanya mazoezi kwa ajili ya kulinda afya ya miili
wakati wa mazoezi ya pamoja kwa Wabunge hao wanawake yaliyofanyika leo
03/02/2017 Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Baadhi ya Wabunge wanawake wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa wameongozana na Spika wa
Bunge (wa pili kushoto) wakifanya mazoezi (Jogging) ikiwa ni sehemu ya
kufanya mazoezi ya pamoja kwa ajili ya kuweka sawa miili, mazoezi hayo
yamefanyika leo 03/02/2017 katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Baadhi
ya Wabunge wanawake wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa
wakifanya mazoezi ikiwa ni sehemu ya kufanya mazoezi ya pamoja kwa ajili
ya kuweka sawa miili, mazoezi hayo yamefanyika leo 03/02/2017 katika
Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
No comments:
Post a Comment