Je ushawahi kupokea
simu ya dharura? Je wewe hujitenga vipi na watu waliokaribu nawe ima ni
mkeo ama hata wafanyakazi wenza ili upokee simu ya kibinafsi?
Na je katika enzi hizi za simu za kisasa au Smartphone wangapi wetu wanatumia simu za kale zisizo na touchscreen?
Haya basi, Hayo sio maswali ya kipima joto ... la!
Rais wa Uganda Bw Yoweri Kaguta Museveni alizua
kioja katika kijiji cha Kyeirumba, wilaya ya Isingiro karibu na mpaka wa
Uganda na Tanzania aliposimamisha msafara wake wa magari ili apokee
simu "ya dharura". Picha za kisa hicho zilipakiwa kwenye mtandao wa
Facebook na afisa wake wa habari Don Wanyama.
Amini usiamini Rais
Yoweri Museveni, alishuka kutoka kwenye gari lake rasmi akachukua kiti
chake na kukiweka kando kando ya barabara mpya ya Isingiro ikipitia
kijiji hicho cha Kyeirumba hadi Tanzania na kupokea simu faraghani.
Mzee Museveni kama vile baba wa taifa alitumia muda wake kufanya shughuli hiyo huku akiwapungia mkono wapita njia.
Baada ya dakika 30 hivi raia wa kijiji hicho walishangaa kuwa miongoni mwa maafisa wakuu serikalini.
Ilikuwa ajabu sana kwao kumuona Museveni akiwa ameketi barabarani.
Waganda katika
mitandao ya kijamii wamesambaza picha hiyo ya rais museveni akizungumza
kwa simu ambayo inaonekana kuwa sio ya kisasa.
Wengine wanamkejeli kwa kuhofia kudukuliwa huku wengine wakimkosoaa kwa kuketi barabarani.
''Kwani hangeweza kupokea simu yake ndani ya gari lake?"
''Ni siri gani hiyo ambayo hakutaka hata walinzi wake wasikie.
''Ama ilikuwa ni #Besigyexit?", wakizungumzia kuachiliwa kwa dhamana kwa kiongozi wa upinzani Dkt Kizza Besigye mapema asubuhi.
No comments:
Post a Comment