TTCL

EQUITY

Sunday, November 23, 2014

Ripoti ya CAG yavuja yakutwa ikisambazwa mitaani ikiwa imenyofolewa kurasa.

Baadhi ya kurasa zinazodaiwa kuchomolewa zawekwa wazi na ripoti nzima yadaiwa itawekwa hewani endapo kutatokea kuchakachua



Taarifa ya mdhibiti na mkaguzi wa  hesabu za serikali  kuhusiana na kashfa ya wizi wa bilioni 321 kwenye akaunti ya tegeta Escrow iliyokabidhiwa kwa katibu wa bunge imekutwa inasambazwa mitaani huku ikiwa imenyofolewa kurasa tatu za mwisho zenye majina ya   waliohusika na mgawo wa fedha hizo kwa lengo la  kutengeneza propaganda ili kuwadanganya wananchi  kuwa taarifa hizo hazijawataja wahusika. 

Akizungumza na  waandishi wa habari mwenyekiti mwenza wa ukawa Mh. James Mbatia  amesema zipo taarifa za baadhi ya waliokuwa   wanasambaza taarifa hizo kuwa wamekamatwa na jeshi la polisi na kuwataka wananchi  kutoa taarifa kituo cha polisi  ili  waweze kuchukuliwa hatua haraka  ambapo amesesistiza  kwamba (UKAWA) wanataka  taarifa hiyo iwasilishwe bungeni kwa ajili ya kujadiliwa Jumatatu .
Mwandishi wetu amemtafuta kamanda wa polisi mkoa wa dodoma  David Misime  na katibu wa bunge Dr.Thomas Kashilillah ambao  wamesema nao wanazisikia  taarifa hizo na wanazifanyia kazi ili kutoa taarifa yao.



Kimsingi, ripoti nzima ipo na itawekwa hewani endapo michezo inayochezwa itaendelea!

Nimesikitishwa na taarifa za kuanza kunyofolewa kurasa za ripoti hii; bahati nzuri kuna watu wanayo original copy na imeshasambaa sana hivyo ni vema wahusika wakaacha wabunge waifanye kazi yao kwa kadiri inavyostahili.

****Cha kusikitisha ni kuwa, Mtu aliyekamatwa akisambaza nyaraka feki za taarifa ya CAG anaitwa Mohamed Mbaruk, ana rekodi ya makosa ya jinai katika mafaili ya Jeshi la Polisi na ni rafiki wa Prof. Muhongo****

Hatungependa kuingilia sana lakini tunaona kama tunalazimishwa kufanya hivyo.

DOKEZO:

Hizi chini ni baadhi ya kurasa zinazodaiwa kunyofolewa...




Quote By MEANDU View Post
Wakati wakihangaika kutawanya taarifa ya CAG iliyonyofolewa baadhi ya kurasa, vyanzo vya habari vya ndani ya BoT vimeleta taarifa muhimu inayoonyesha uhusikaji wa mamlaka mbalimbali katika kuagiza malipo ya escrow yafanyike.

Maelezo yanatoa sura ya uhusikaji wa moja kwa moja wa ofisi ya Werema (na Werema mwenyewe) kushawishi BoT kulipa.Maelezo zaidi yanaonyesha hata Kikwete aliagiza BoT ilipe akinukuu ushauri wa Werema.

Hapo chini ni baadhi ya utetezi wa BOT. Utetezi kamili wenye kurasa 12 download attachment hapo chini



No comments:

Post a Comment