Wana kijiji watano
katika eneo lililokumbwa na ukame kaskazini mwa India wamefariki
wakijaribu kutafuta maji katika kisima kisichotumika.
Wanaume hao
walifariki baada ya kuvuta gesi ilio na hewa chafu ambayo ilikuwa ndani
ya kisima hicho katika jimbo la Haryana kulingana na afisa mmoja.Eneo kubwa la India linakabiliwa na ukame mbaya ambao umewaua takriban watu 300.
Haryana na majimbo mengine wiki iliopita yalikosolewa na mahakama ya juu nchini India kwa kushindwa kutambua tatizo hilo la maji.
Lakini naibu afisa wa polisi katika wilya hiyo Virender Singh alikana kwamba walihitaji maji ya kunywa akisema wanaume hao walitaka kukitumia kisima hicho kwa maji ya kuoga na kuosha.
''Kisima hicho kilikuwa hakijatumika kwa takriban miaka mitano hadi sita na gesi yenye sumu ilikuwa imetanda huko chini'',aliambia kituo cha habari cha AFP.
No comments:
Post a Comment