Tanzania imewasilisha leo ripoti yake ya miaka
minne ya utekelezaji wa haki za binadamu kwa Umoja wa Mataifa mjini
Geneva nchini Uswisi, ambapo imeeleza kupiga hatua katika maeneo kadhaa
ikiwamo elimu.
Mwakilishi wa Kudumu wa nchi Tanzania, katika ofisi za Umoja wa Mataifa mjini Geneva, Balozi Modest Mero,(kulia).
Mwakilishi
wa kudumu wa nchi Tanzania, katika ofisi za Umoja wa Mataifa mjini
Geneva, Balozi Modest Mero, amesema licha ya changamoto kadhaa za
ukosefu wa fedha amesema serikali ya Tanzania imetekeleza karibu
asilimia 50 ya maelekezo kama walivyoshauriwa katika ripoti ya awali.
Balozi Mero amesema kuwa katika ripoti hiyo imeonyesha changamoto
nyingine ambazo zimefanywa kushindwa kufikia malengo kamili kutokana na
kushindwa kuridhia baadhi ya sheria za Kimataifa ambazo zinakinzana na
sheria za ndani ya nchi.
Kuhusu mjadala wa kuminya haki ya mawasiliano kufuatia kupitishwa
sheria ya mtandao nchini Tanzania, Balozi Mero amesema kuwa sheria hiyo
ipo duniani kote kutokana na malengo yake makuu ikiwemo kuzuia uhalifu
ikiwemo ugaidi na matukio mengine ya uvunjifu wa amani.
No comments:
Post a Comment