Katika
Dunia tuishiyo sasa binadamu hatuko peke yetu, lakini tumejijengea
dhana kuwatunaishi peke yetu huku tukisahau kuwa Mungu kaumba viumbe
kadha wa kadha vinavyoonekana na visivyoonekana.
Unaweza
kushangaa ama kudhani kuwa namaanisha juu ya uwepo wa nguvu za kigiza,
La Hasha!, mtu anapokuuliza kwamba Je unafahamu maana ya neno ‘UFO’ (Unidentified Flying Object)? Bila shaka watu wengi watakuwa hawafahamu kuhusiana na vitu hivi na wengine wanaweza kukupa maana nyingine tofauti na mada.
Neno
UFO limechukua kasi kwenye vyombo vya habari vingi duniani hasa vya
wenzetu wa nchi za Magharibi, pia upande wa Asia ambapo baadhi ya
Wataalam wamajaribu kufuatilia kwa karibu juu ya vitu hivi na wapi
vimetokea na madhumuni ya kuonekana ovyo katika maeneo tofauti na
madhara yake lakini hakuna maelezo mazuri yanayoweza kuelezeka katika
hilo, na hii imepelekea wataalam hao kuziita baadhi ya tafiti zao kuwa
ni zisizoelezeka (Unexplained files about UFOs)
Ebu tujiulize maswali UFOs ni vitu gani, na malengo yake kuonekana duniani ni nini haswa?
UFOs
ni Vyombo vyenye ukubwa tofauti na maumbile tofauti ambapo vingine
vinakadiliwa kuwa na ukubwa wa futi 100 ama zaidi vingine na muonekano
wake ni wa duara kama sahani kubwa la chuma lenye kung’aa (steel
shaped-saucer), lakini pia vinaweza kuwa na umbo mengine tofauti kama
vile maumbile ya pembe tatu ambapo kwa chini zinakuwa ya na taa zenye
kutoa miale mikali ya mwanga yenye rangi ya bluu, nyekundu na nyeupe.
UFOs
ndizo zinabeba viumbe wajulikanao kama Aliens na viumbe hawa wanamaumbo
kama ya binadamu lakini tofauti yake iko katika macho na vidole kwani
viumbe hawa wana macho makubwa yenye umbo la ovali, vidole vikubwa
vitatu badala na wakati mwingine mikono mirefu, na miili yao ni kama
yenye hali ya mpira hivi na wakati mwingine waonekanapo wanakuwa kama
waliovalia aina ya kama nguo zenye kubana mwili mzima zenye rangi ya
bluu na mikanda viunoni mwao, hakika viumbe hivi vinatisha kimuonekano
wao.
Taarifa
zisizo rasmi kutoka kwenye vyombo mbalimbali vya habari na maelezo ya
watafiti mbalimbali ulimwenguni vinaeleza kuwa UFO hutumika kama chombo
cha anga cha kusafiria kwa viumbe hao ambao wanasemekana kutoka katika
sayari ya mbali na ni viumbe wenye akili kuliko binadamu wa kawaida.
Vyombo
hivi viko tofauti na vyombo vyetu vya anga kama vile ndege za abiria au
roketi ziendazo mwezini, kwani tofauti iliyopo hapa ni kwamba vyombo
hivi vibebavyo viumbe hao vinasemakana kuwa na kasi ya ajabu tofauti na
kifaa chochote cha hapa duniani kuwa na mwendo kasi kama huo, lakini pia
UFO CRAFTS zinaweza kubadili mwelekeo wake katika nukta yoyote ya
safari yake wakati wowote na kuweza kutoweka machoni ndani ya sekunde.
UFO
pindi zifikapo katika uso wa dunia hazitoagi kelele na zinatabia ya
kuacha nguvu fulani ya umeme wenye usumaku (Electromagnetic Radiation)
ambayo wakati mwingine inaweza kusababisha hitilafu ya umeme wa kawaida
tuutumiao, maajabu mengine ni kwamba pindi vikiwa vimetua sehemu fulani
basi mfumo mzima wa mawasiliano kama vile ya simu, rada, na wakati
mwingine majira ya saa zetu huathiriwa na kwenda kinyume (anticlockwise)
na endapo umeme utokanao na nguvu ya usumaku ikiwa iko juu basi moto
unaweza kujiwakia popote iwe ndani ya nyumba zetu ama nje hata kwenye
maji pia.
Tukio
kama hili liliwahi kutokea mnamo Januari 2004 nchini Italia katika
kijiji cha Canneto (Caronia) ambapo nyumba za watu zikiwemo samani zao
zikiwaka moto licha ya umeme katika kijiji hicho kuzimwa, bado ulizidi
kushika kasi na ulikuwa ukiwaka wenyewe toka nyumba moja kwenda
nyingine, runinga, friji, majiko yalikuwa yakiwaka moto bila kuwashwa,
pia mifumo ya simu nayo haikuweza kufanya kazi, mifumo ya magari ilikuwa
ikijiwasha na kujizima yenyewe bila kuwashwa pamoja na honi za magari
zikijipiga zenyewe, ama kweli haya yalikuwa ni maajabu katika eneo hilo
ambapo baada ya uchunguzi wa muda mrefu uliogharimu fedha nyingi na
Wataalam wengi ilikuja kubainika kuwa Aliens ndiyo chanzo kikubwa cha
moto katika kijiji hicho.
Katika
baadhi ya matukio yanayohusiana na uwepo wa UFOs, watu ambao wamekuwa
wakisafiri na magari yao pindi wakutanapo na vitu hivyo basi magari
yalizimika papo hapo na kushindwa kuwaka na wakati mwingine katika
nyakati za usiku, miale ya taa za magari yao ilipinda ghafla na kuelekea
katika eneo ambalo UFO imetua lakini hii yote inatokana na nguvu zisizo
za kawaida kutoka katika UFOs.
Je, kuna ukweli wowote juu ya madai ya uwepo wa UFOs?
Asilimia
72 ya wananchi wa Marekani wanaamini juu ya uwepo wa uhai nje ya Dunia
na kwamba kuna viumbe wengine wanaishi huko. Baadhi yao wanaamini juu ya
uwepo wa UFOs na huku wengine ambao ni wahanga wanaamini kuwa wamewahi
kukutana nazo katika mazingira tofauti. Kuna wengine pia wanamadai kuwa
wao wamewahi kutekwa na viumbe hao (alien abductions) na kuingizwa
kwenye UFO na baadaye kurejeshwa walipo kuwa.
Baadhi
ya watu ambao wanatoa madai ya kuwahi kutekwa na Aliens, wengi wao
wanasimulia kuwa mara walipokutana na UFOs njiani walijikuta ghafla
wakiota ndoto na mara wakajikuta wako katika eneo wasilolijua na kulazwa
katika vitu kama vitanda na kuchunguzwa na viumbe hao, lakini wengine
wamekuwa wakiugua vichwa kwa muda wa wiki nzima pindi walipokutana na
aliens huku wengine wakipoteza kumbukumbu kwa muda wa wiki moja na
baadaye kurejea katika hali zao za kawaida.
Tarehe
18 Aprili, 1961 Eagle River Wisconsin nchini Marekani, Mkulima na
Mfugaji ajulikanaye kama mzee Paul Simonton aliwahi kuona kitu chenye
umbile la Sahani kubwa la chuma (UFO) ambayo ilitua katika shamba lake
mara juu ya chombo hiko pakafunguka, wakati hayo yakitokea, mzee huyo
aliamua kuisogelea kuona ni kitu gani haswa kikiendelea na hapo ndipo
akaviona viumbe vitatu vyenye maumbile kama ya binadamu vilionekana
vikihitaji maji ndipo yule mzee akachukua jagi lenye maji na kuwapa wale
viumbe, cha ajabu nao wale viumbe wakampatia vipande vinne vya keki (4
pancakes) ambavyo hapo baadaye baada ya uchunguzi wa Maabara ilibainika
kuwa vipande vile vilitengenezwa kwa kutumia mafuta mazito yaani grisi
na unga usiojulikana na usio na radha, tukio hili lilikuwa la ajabu
kutokea nchini humo.
Kumekuwepo
pia na taarifa lukuki juu ya uwepo wa UFOs kutoka kwenye mitandao
mablimabli, magazeti, majarida, kutoka kwa watu waliowahikuona UFOs,
walio waona Alliens, mpaka wale waliowahi kutekwa na kuwekwa kwenye UFO
Crafts madai haya yote wakati mwingine inakuwa ni vigumu kuyathibitisha,
kwani muda mwingine taarifa hizi zinakuwa kubwa kushinda tukio lenyewe,
wakati mwingine kwa makusudi zinakuwa ni taarifa za kutengeneza
(propagandas) au zenye upotoshaji kwa umma, lakini bado kuna wakati
tukio moja linakuwa na mashahidi zaidi ya mmoja, linakuwa limeacha
ushahidi wenye kuonekana yaani ushahidi unaoweza kuugusa kwa mkono,
ushahidi ambao ni zaidi ya maneno ya shuhuda mwenyewe.
Hivyo,
Katika historia ya vitu hivi na maajabu yake UFOs kwa wanahistoria
zinasemakana kurekodiwa kwenye majalada ya historia tangu enzi na enzi
ya historia ya mwanadamu, ingawa suala hili halipo kwenye mitaala ya
somo la historia lenyewe, na hivyo baadhi ya watu huamini kuwa hakuna
kitu kama hicho.
Kuanzia
mwaka 1991 mpaka 1993 jiji la Mexico lilifunikwa na taarifa za
kuonekana kwa UFOs ukiwemo mwezi wa Julai 11, 1991 ambapo watu 17 ambao
hawana mahusiano yoyote katika maeneo tofauti ya jiji hilo wakiwa na
kamera zao, waliweza kunasa picha ya sahani kubwa lenye mnga’o wa chuma
karibu kabisa na usawa wa jua mbalo muda mfupi nyuma lilikuwa limepatwa
na mwezi. Diski hilo lilikuwa limening’inia angani kwa muda bila kusogea
upande wowote ule. Lakini watu hawa hawakujua kama wamepiga picha UFO
mpaka watu wengine walipo ng’amua wakati wanaonesha video hizo.
Baadaye
baadhi ya Watafiti ndipo wakaanza kupokea video na picha nyingi zinazo
onesha umbo la duara kubwa la chuma (UFO) zikiwa kwenye anga la Mexico
ambazo picha zake zilipigwa na watu tofauti. Vyombo vya rada na hata
marubani kadhaa wamewahi kuripoti ama kuviona vyombo hivyo vikiruka
katika anga la Mexico.
Kutoka
kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa (Benito Juárez International
Airport) Machi 4-5, 1992 tukio la kuonekana kwa UFO liliwahi kuripotiwa
na kuthibitishwa na rada ya uwanja huo juu ya kuonekana kwa vitu
hivyo.
Mexico
imekuwa na historia ndefu ya kuonekana kwa UFOs na nyingi kati ya hizo
zimekuwa zikidharauliwa na wana sayansi huku wakisema kuwa ni vipande
vya uchafu ama vumbi kutoka kwenye anga, roketi za kivita, maputo ya
hali ya hewa ama uzushi.
Taarifa
zinaeleza kuwa wakati mwingine UFOs vilikuwa vikifukuzwa na ndege ya
doria baada ya kudhaniwa kuwa ni ndege za wabeba dawa za kulevya, lakini
ghafla ziliweza kutoweka na zilipo onekana tena zilikuwa zimeizingira
ndege hiyo ya doria ya jeshi la anga la Mexico.
Mtafiti
kwenye masuala ya UFOs, Bwana Brit Elders anazungumzia suala la UFOs
kunaswa kwenye rada kwenye jiji la Mexico, “Rada ya Mexico imefuatilia
na kurekodi UFO sawa na yale yanayosemwa na watu waliowahi kuona kwa
macho yao wenyewe kutoka ardhini na kutoka kwa marubani wa ndege wakiwa
angani”, alisema Elders.
Katika
tukio hilo, Serikali ya Mexico iliposhinikizwa na wadau mbalimbali juu
ya kulifanyia uchunguzi suala tukio hilo ambapo Serikali hiyo ilifanya
mkutano na waandishi wa habari na kufafanua kuwa, Serikali hiyo
ilitambua juu ya kuonekana kwa vitu hivyo lakini ikasisitiza kuwa UFOs
hazina madhara yoyote kwa wananchi.
Tukio
jingine la mwezi Machi 13, 1997 katika Jimbo la Arizona kwa dakika 106
mida ya saa mbili na robo usiku lilishuhudia kile ambacho baadaye
kilijulikana kama ni UFO. Baada ya tukio hilo simu zilimiminika kwenye
vituo vya dharura vya jimbo hilo kutoka kwa mashuhuda wa maeneo kadhaa
ikiwemo Prescott, Wickenburg, Glendale, Phoenix, Scottsdale na Tempe.
Kutoka
kwa mashuhuda hao, ni kuwa chombo hicho kilikuwa karibu kabisa na kituo
cha Luke Air Force, ambapo ndege aina ya Falcon Super Hornets (F-16)
tatu zilitoka kwenda kufuatilia chombo hicho kujua ili kuweza kujua
kulikoni, lakini ndege hizo za kijeshi mara zilipokaribia chombo hicho
kilitoweka ghafla kama kupepesa mboni ya jicho. Hata hivyo baadhi ya
maafisa wa kituo hicho cha Luke kama ilivyo tegemewa walikataa kuwa
hakuna ndege za kijeshi zilizotolewa kwenda kukifuatilia chombo hicho na
wala hawafanyi tafiti juu ya uwepo wa UFOs.
Peter
Davenport toka Kituo cha Taifa cha kutoa Taarifa za UFOs kilichopo
Seattle, Washington, alipokea mamia ya simu kuhusiana na tukio hilo na
maoni yake binafsi yalikuwa hivi,
“Tukio
la Arizona lilikuwa wazi kabisa kati ya matukio niliyopata kuyaona,
tulicho kiona pale ni kitu cha kweli kabisa. Tayari wako hapa viumbe
kutoka sayari nyingine”, alisema Davenport.
Miezi
mitatu baada ya tukio, Juni 18, 1997 tukio hilo lilianza kuzungumziwa
kwenye vyombo vikubwa vya habari duniani na kuanza kupata mvuto na
kuvuta hisia za watu. Liliripotiwa kwenye NBC, MSNB, CNN na ABC.
Barani
Afrika, tukio la kuonekana kwa UFOs liliwahi kuripotiwa katika baadhi
ya vyombo vya habari vichache nchini Zimbabwe, Mwandishi Cynthia Hind
aliandika kuwa mnamo tarehe 14 Septemba Ruwa, Zimbabwe vilitua vitu
ambavyo vinafanana na UFOs katika shule moja na tukio hilo lilishuhudiwa
na wanafunzi wenye umri mdogo (kati ya 5-12) ambao walikuwa wakicheza
nje ya uwanja wa shule kipindi walimu wao wakiwa kwenye Mkutano, na siku
mbili baada ya tukio hilo (yaani 16 September, 1994) Mwandishi huyo
akaamua kuwafanyia usaili wale watoto wote wa shule kwa kuwaambia
wachore kitu ambacho walikiona siku ya tukio, huku kila mtoto akiwa peke
yake waliweza kuchora mfano wa kitu walichokiona na hapo ndipo wale
watoto wakachora michoro ambayo iliweza kufafana jambo hilo lilimfanya
mwandishi huyo kubaini kuwa ni UFOs ilitua katika eneo hilo na huku
ikiwa imefuatana na vitu vingine vinne.
Kwa
takribani miaka hamsini sasa tangu Serikali mbalimbali duniani na
watafiti walipoamua kulishughulikia suala la UFOs na kutafuta majibu ya
maswali kuhusiana na asili yake hasa ni nini na tija au madhara yake kwa
binadamu waishia katika sayari ya Dunia ni yapi lakini hakuna kati ya
hao waliokuja na majibu ya kuridhisha ama majibu rasmi kuhusiana na
suala la hilo.
Basi
kama UFOs zitakuwa ni kweli zipo, na asili yake hasa ni kutoka nje
aidha ya sayari yetu ama galaxy yetu, ukweli huo hakuna shaka utakuwa ni
changamoto ya namna yake kwa binadamu wote na Kwa upande mwingine ikiwa
UFOs ni si kama hivyo tunavyoambiwa ama si hivyo inavyoelezewa na wale
walio wahikushuhudia , basi vyombo hivyo vitakuwa ni ushahidi tosha wa
mpango kabambe ambao mabilioni ya binadamu hawafahamu hatima na malengo
yake ni nini na ambao athari yake huenda ikamuathiri kila binadamu
aliyepo kwenye sayari hii.
No comments:
Post a Comment