Kampuni
ya Tigo Tanzania imetoa msaada wa madawati 400 yenye thamani ya
shilingi milioni 66 kwa shule nane za msingi katika manispaa ya Mwanga,
mkoa wa Kilimanjaro, ikiwa ni mchango wa kampuni hiyo katika kuisaidia
serikali kukabiliana na upungufu wa madawati katika shule za msingi
nchini.
Akizungumza
leo katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika shule ya msingi
Reli Juu katika manispaa ya Mwanga, Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya
Kaskazini George Lugata amesema mchango huo ni sehemu ya utekelezaji wa
dhamira ya kampuni hiyo ya kuunga mkono jitihada mbalimbali za kuleta
maendeleo nchini.
“Mchango
huu ni sehemu ya jitihada mbalimbali zinazofanywa na Tigo katika
kusaidia utekelezaji wa miradi yenye tija kubwa kwa jamii. Tunaamini
kwamba kupitia msaada huu, Tigo inatoa mchango wake katika kujenga
viongozi wa baadaye wa taifa hili na wanataluuma mbalimbali wakiwamo
madaktari, wahandisi na wengineo, “amesema Lugata.
Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro, Meck Sadiki akikabidhi madawati 400 yenye
thamani ya shilingi milioni 66 kwa Mwenyekiti wa halmashauri ya Mwanga,
Theresia Msuya yaliotolewa na Kampuni ya Tigo, Kulia ni Mkurugenzi wa
Tigo Kanda ya Kaskazini George Lugata.
Lugata
amesema mwaka jana Tigo ilikabidhi msaada kama huo wa madawati katika
shule za msingi katika mikoa ya Shinyanga, Mbeya Iringa na Morogoro na
kuongeza kwamba kampuni hiyo itaendelea kutoa madawati zaidi sehemu
mbalimbali nchini siku za zijazo.
Makabidhiano
yalihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro mheshimiwa Meck Sadiki
ambaye alisema madawati hayo 400 yataboresha mazingira ya kujifunzia kwa
watoto katika Mkoa wa Kilimanjaro na kutoa wito kwa wadau wengine
kuunga mkono zoezi hilo.
Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro, Meck Sadiki (Kulia), akiwa katika picha ya
pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mwanga Theresia Msuya (katikati)
Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini George Lugata.
“Tunapenda
kutoa shukrani zetu za dhati kwa kampuni ya Tigo kwa kuwa mdau muhimu
kwetu katika jitihada zinazoendelea za kujaribu kupunguza tatizo la
ukosefu wa madawati ya kutosha katika shule za msingi za mkoa wetu wa
Kilimanjaro. Ni dhahiri kwamba msaada huu wa madawati 400 yatawawezesha
mamia ya wanafunzi wetu kupata sehemu za kukaa na hivyo kujipatia elimu
zao katika mazingira bora zaidi,” alisema Sadiki.
Madawati hayo yametolewa kwa shule za msingi nane kama ifuatavo, Mramba,Kawawa, Mwanga, Naweru,Kiboriloni, Lawate na Reli Juu.
No comments:
Post a Comment