Wizara ya Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano imetoa wito kwa wananchi na wadau mbalimbalikuendelea
kutoa maoni na mapendekezo ili yatumike kuboresha Sera mpya ya Taifa ya
Habari Teknologia ya Mawasiliano(TEHAMA) ya (2016) ili kuisaidia
serikali kutatua changamoto za upatikanaji wa habari na mawasiliano
katika jamii
Wito huo umetolewa jijini Mbeya
na Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia maswala ya simu katika Wizara
ya Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano Ndugu John Mwera wakati wa zoezi la
uchukuaji maoni lililofanyika katika viwanja vya chuo cha Uhasibu (TIA)
jijini Mbeya
Amesema Teknolojia ya habari
na mawasiliano hapa nchini imekuwa ikikua kwa kasi kubwa katika kipindi
cha miaka kumi tangu serikali ilipotunga sera kwa mara ya kwanza mwaka
2003.
Amesema hali hiyo imechangia
kuwepo kwa miundombinu ya huduma za mawasiliano kila mahala na
kufanya matumizi kuwa makubwa ambapo Zaidi ya watu milioni 39 wanatumia
mawasiliano ya simu hivyo kufanya kuibuka kwa changamoto mbalimbali
katika sekta hiyo.
Amesema ili kufahamu changamoto
wanazo kutananazo wananchi pamoja na mtizamo wao katika utumiaji wa
mawasiliano, wizara hiyo imeamua kuweka utaratibu wa kuweka vituo vya
kukuza ubunifu katika jamii katika kila mkoa ambapo kila mwananchi
anakuwa huru katika kutoa maoni yao na ushauri ili kuisaidia serikali
katika kupanga mikakati ya kuweza kuzitatua changomoto hizo.
“Huwezi kukaa ofisini ukatunga
sera ambazo haziwahusu mwananchi wa kawaida hivyo lazima twende kwa
wananchi na kujua wanahitaji nini ili kutunga sera na kuweza
kuzitatua”Alisema Mwela.
Aidha amesema kuwa kila maoni yanayotolewa na wananchi serikali inayathamini katika kuweza kutoa muelekeo wa sekta
ya mawasiliano kwani sekta hiyo bado inamchango mkubwa sana katika kutoa
huduma mbalimbali kwa wananchi.
Hata hivyo amesema bado wizara
inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni elimu ndogo kwa waanchi
juu ya utunzaji wa miundombinu ya sekta ya mawasiliano hususani mkongo
wa taifa
sanjali na wizi wa mafuta
kwenye minara ya simu hivyo amewataka wananchi kuwa walinzi wa
miundombinu hiyo ili kuendelea kukuza sekta hiyo sanjali na kulahisisha
upatikanaji wa huduma kwa jamii. Amesema zoezi hilo la uchukuaji maoni
kwa wananchi juu ya uboreshaji wa sera ya TEHAMA itaendelea inchi nzima
katika mikoa yote ya Tanzania bara na Visiwani.
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Cha Uhasibu Jijini (TIA)wakijibu baadhi ya Maswali kama sehemu ya ukusanyaji maoni ili kuboresha sera ya TEHAMA . |
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Cha Uhasibu Jijini (TIA) na wadau mbalimbali kutoka Mkoani Mbeya wakijibu baadhi ya Maswali kama sehemu ya ukusanyaji maoni ili kuboresha sera ya TEHAMA . |
No comments:
Post a Comment