Mkurugenzi wa LHRC Dkt. Hellen Kijo - Bisimba
Kituo
cha Sheria na Haki za Binadamu nchini Tanzania (LHRC) kimeitaka
serikali kuweka mfumo maalum wa kushughulikia matatizo ndani ya nchi.
Mkurugenzi wa LHRC Dkt. Hellen Kijo-Bisimba ametoa kauli hiyo leo
jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na East Africa Television na
East Africa na kuainisha kuwa ni lazima kuwe na mfumo maalum ambao
utaweza kusaidia mambo yaende kwa kufuata sheria na Katiba ya nchi
ilinavyoelekeza.
Amesema Rais Dkt John Pombe Magufuli ameanza kutekeleza mambo ambayo
makundi ya kutetea haki za binaamu waliyapigania kwa miaka mingi na
hayakuweza kutekelezwa kwa wakati huo kutokana na kuwepo kwa usimamizi
mbovu kwa baadhi ya sekta mbalimbali nchini hivyo ni vema kuwa na
uangalifu wa hali ya juu katika utekelezaji wake.
Amesema kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinamuunga mkono rais
Dkt. Magufuli na kituo cha LHRC kina nia njema na wananchi wa Tanzania
pamoja na serikali yake ndiyo maana kituo kimekuwa mstari wa mbele
kusimamia haki itendeke kwa kuzingatia mfumo na utawala wa sheria ya
nchi inavyoelekeza.
Kwa upande mwingine Dkt. Kijo - Bisimba amesema kitendo kinachofanywa na
kambi ya upinzani Bungeni cha kutoka kwenye baadhi ya vikao vya Bunge
ni aina mojawapo ya uwasilishwaji wa jambo fulani hivyo ni lazima
wanasiasa watumie njia ya Kidemokrasia katika kuwatumikia wananchi wake.
No comments:
Post a Comment