Wanne kutoka kulia, Waziri
Ummy Mwalimu akipokea hundi ya sh.
Mil 220, iliyotolewa na taasisi ya BAPS Charity kwa ajili ya kusaidia
matibabu ya watoto 101, wa magonjwa ya moyo waliopo katika taasisi ya
JKCI.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Ally
Mwalimu leo Machi 2.2016, amepokea msaada wa fedha kwa ajili ya
kuwezesha matibabu ya wagonjwa wa moyo katika taasisi ya Moyo ya Jakaya
Kikwete (JKCI) ambapo kwa msaada huo, jumla ya watoto 101,
wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa moyo katika taasisi hiyo kwa gharama
za fedha hizo zilizotolewa na Jumuiya ya Kihindu waishio Dar es Salaam
ijulikanayo kama BAPS Charity, kwa kuguswa kwao na kutoa msaada mkubwa
na upendo waliouonyesha kwa watanzania wanaosumbuliwa na maradhi ya
moyo.
Wiziri
Ummy amebainisha kuwa, kiasi cha msaada unaotolewa utawezesha wagonjwa
wapato hao kupatiwa matibabu ya moyo hivyo kuwa, faraja kubwa kwa
wagonjwa waliokuwa wakisubiria huduma hizo kwa muda mrefu kutokana na
kushindwa gharama za matibabu yake.
Aidha,
kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)
iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Mohamed
Janabi amepongeza kwa msaada huo kwani utasaidia kutoa matibabu kwa
watoto hao 101, huku pia taaisi yake ikikabiliwa na changamoto ya
wagonjwa wengi ambapo amezitaka taasisi na wadau wengine kujitokeza
kuchangia ilikupunguza wagonjwa wanaosubiria kupatiwa matibabu hasa
upasuaji.
Prof.
Janabi ameeleza kuwa, matibabu ya wagonjwa wa moyo yana gharama kubwa
kwani kwa mtoto mmoja ndani ya nchi yanafikia hadi Milioni nne (Mil 4)
huku kwa nje ya nchi matibabu hayo yakifikia hadi Milioni 16, gharama
hizo ni kubwa hivyo wadau na taasisi binafsi zimeombwa kujitokeza
ilikuokoa maisha ya wagonjwa wengi hasa watoto ambao wapo katika taasisi
hiyo na mikoa mingine.
Kaimu
Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Mohamed Janabi akisoma
taarifa fupi juu ya magonjwa wagonjwa wa moyo wanaopatiwa matibabu
katika taasisi hiyo na namna walivyojipanga kutoa matibabu ya upasuaji
kwa watoto hao 101, waliolipiwa gharama za matibabu kutoka BAPS Charity.
Wengine ni Waziri wa Afya, Mh. Ummy Mwalimu pamoja na viongozi wa BAPS
Charity.
Waziri
Ummy Mwalimu akiongea na mmoja wa wazazi waliokuwa katika tukio hilo la
kukabidhiwa fedha kiasi cha Mil 220, kwa ajili ya wagonjwa wa moyo 101,
ambao wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji katika taasisi ya JKCI.
Waziri
wa Afya, Ummy Mwalimu akipata kumjulia hali mtoto Zahara Seleman Muna
(10) ambaye anasumbuliwa na magonjwa ya moyo. Hata hivyo Waziri Ummy
Mwalimu amejitolea kama Waziri kuhakikisha atawasaidia watoto hao katika
kutimiza ndoto zao ikiwemo kuwasomesha na masuala mengine kupitia
Wizara yake ambayo yenye dhamana, Waziri Ummy aliguswa na watoto hao
kutokana na ndoto zao walizokuwa nazo ikiwemo kusoma zaidi.
Mwenyekiti
wa taasisi ya BAPS Charity, Subhash Patel, akizungumza machache
kuhusiana na mchango huo wa Milioni 220, kwa ajili ya matibabu ya watoto
101, ambapo pia aliomba wadau wengine kujitokeza kuchangia ilikuisaidia
Serikali katika kuhakikisha uhai kwa wagonjwa wa moyo hasa watoto hapa
nchini.
Bw.
Alfred D. Dafi mkazi wa Karatu akiwa amembeba mtoto wake, Beatrice
Alfred (13) akitoa shukrani zake kwa Waziri wa Afya, Mh. Ummy Mwalimu
kwa kuweza kuchukua majukumu ya kumsaidia mtoto wake katika masuala ya
kumsomesha na mambo mengine kama Waziri mwenye dhamana. Waziri amechukua
jukumu ya kuwasaidia watoto hao, kutokana na kuguswa na ndoto
walizonazo ikiwemo kusoma wafike mbali. Mtoto huyo Beatrice hadi sasa
anasoma darasa la sita, katika shule ya Sumawe, iliyopo Karatu.
Dk.
Naiz Majani, ambaye ni daktari wa watoto wa magonjwa ya moyo akitoa
ufafanuzi kwa wanahabari juu ya matatizo ya magonjwa ya moyoo ambapo
amebainisha kuwa kati ya asilimia 10, pekee magonjwa ya moyo yanabainika
kwa mwanamke huku miongoni mwa wazazi wanaozaa watoto wenye matatizo
ya moyo ni wale waliokosa chanjo mbalimbali ikiwemo ya Lubela na mambo
mengine.
Watoto
Beatrice Alfred (13) na Zahara Seleman Muna (10) wakiwa katika picha ya
pamoja. Waziri wa Afya, Mh. Ummy Mwalimu ameamua kujitolea kuwasaidia
kutimiza ndoto zao ikiwemo suala la kuwasomesha na mahitaji mengine kama
Waziri mwenye dhamana. Kushoto ni Baba wa mtoto Beatrice, Bw. Alfred
Dafi ambaye anatokea Karatu.
Waziri
Ummy Mwalimu akimpa pole dada wa Zahara Seleman Muna (10), Editha
Foi,(kulia) aliyekuwa akilia kwa uchungu baada ya Waziri Ummy Mwalimu
kuamua kujitolea kuwasaidia watoto hao iliwatimize ndoto yao ya elimu na
mahitaji mengine kama Waziri Mwenye dhamana.
No comments:
Post a Comment