Baada ya kuendelea kushamiri kwa matukio ya ujambazi
nchini, waziri wa mambo ya ndani Mhe. Charles Kitwanga ametoa onyo kali
kwa majambazi hao.
Akizungumza
katika kipindi cha East Africa Drive kinachorushwa kupitia East Africa
Radio Waziri wa Mambo ya Ndani amesema kwa sasa wamejipanga vya kutosha
kukabiliana na majambazi hao na kuhakikisha wanadhibiti masuala ya
uharifu ambayo kwa siku za karibuni yamezidi kuongezeka kwa kasi.
"Tumejipanga vizuri na watakaporudia hatatoka mtu waambieni wapelekeeni ujumbe kwamba watakao thubutu tena hatatoka yoyote kati yao" Amesema Waziri Charles Kitwanga.
Siku ya jana jeshi la polisi mkoa wa Arusha lilithibitisha kuwaua kwa risasi watu watatu wanaodaiwa kuwa ni majambazi na kukutwa na bunduki moja aina ya AK 47 ikiwa na risasi kumi na nane milipuko ishirini na saba, sare za jeshi la wananchi wa Tanzania na bendera inayodaiwa kutumiwa na kikundi cha Al Shabaab.

No comments:
Post a Comment