(Mitandao ya kijamii) Facebook, Whassap zazimwa Uchaguzi wa Uganda
Mitandao ya kijamii imezimwa hii leo nchini
Uganda wakati wa zoezi muhimu la kuchagua Rais pamoja na wabunge wa
kuwawakilisha wananchi.
Rais
wa nchi hiyo Yoweri Musevrni amenukuliwa akisema kuwa mitandao hoyo
imezimwa kwa lengo jema la kuzuia kusambaza taarifa za uongo na za
kichochezi ambazo zinaweza kusababisha matatizo katika taifa hilo.
Kituo kimoja cha uchaguzi uchaguzi wake umesitishwa jijini Kampala
baada ya kutokea kutoelewana baina ya wananchi na askari waliokuwa
wakilinda amani na usalama.
Aidha Mgombea Urais Dkt. Kiza Besgye amesema haamini kama uchaguzi
huo utakuwa huru na haki kuanzia upigaji kura hadi upatikanaji wa
matokeo.
Mjini
Kampala, ambapo makao makuu ya Tume ya Uchaguzi yapo, bado kuna vituo
ambavyo kufikia saa nne upigaji kura haukuwa umeanza.
Hata hivyo,
tume hiyo kwenye ukurasa wake wa Twitter, imeandika: "Tunabaki kuwa na
matumaini na tunawahikishia kwamba nyote mtaweza kupiga kura leo.
Tunasikitika kutokana na kuchelewa huku. Asanteni.”
Kuhusu iwapo
muda wa kupiga kura ungeongezwa, tume hiyo kupitia mitandao ya kijamii
ilisema kwa mujibu wa sheria, ni sharti vituo vifungwe saa kumi alasiri.
Raia katika maeneo mengi nchini humo pia
wamelalamikia kutatizika wakiingia mitandao ya kijamii kama vile
Twitter, Facebook na WhatsApp, kwa kutumia simu. Serikali
haijaeleleza ni nini chanzo cha matatizo hayo.
Kuna wagombea saba wa urais wanaojaribu kuhitimisha uongozi wa Rais Yoweri Museveni ambaye ameongoza kwa miaka 30 sasa.
Wanaotoa ushindani mkubwa kwa Bw Museveni ni mgombea wa FDC Kizza Besigye na waziri mkuu wa zamani Amama Mbabazi.
Kuna jumla ya wapiga kura 15 milioni ambao wamejisajili kupiga kura nchini humo kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi.
No comments:
Post a Comment