Mkuu wa kanisa
katoliki duniani Papa Francis amesema kuwa wazo la mgombea wa kiti wa
chama cha Republican nchini Marekani , Donald Trump la kujenga ukuta
kati ya Mexico na Marekani si ukristo.
Papa Francis alisema kuwa
kwa mtu yeyote ambaye katika karne hii ya 21 anayetaka kujenga ukuta
badala ya kujenga daraja huyo si mkristo
Kiongozi huyo wa kanisa katoliki aliyasema hayo katika siku yake ya mwisho ya ziara nchini Mexico.
Trump
ambaye anapigiwa upatu kutwaa tikiti ya chama cha Republicans katika
uchaguzi mkuu ujao amependekeza kujenga ukuta na ua katika mpaka kati ya
nchi yake na mexico ilikuwazuia wahamiaji kuingia nchini Marekani.
Licha ya kuwaambia waumini wa kanisa Katoliki kuwa
hatawazuia kutumia uhuru wao kumchagua rais wanaompenda, papa Francis
amesema kuwa iwapo Trump anapanga kujega ua basi ''si mkristo''
Hilo haliambatani na mafunzo ya injili
"sharti tutathmini matamshi yake '' tunapaswa kuchunguza kwa kina ''
Bwenyenye
Donald Trump kwa upande wake amesema kuwa papa Francis hana haki yeyote
kumhukumu iwapo ni muumini au la ''inasikitisha'' alisema Trump.
Mtazamo huo wa papa Francis bila shaka unatarajia
kuwapa wapinzani wa Trump fataki huku wakiendelea na kura za mchujo
ambapo msimamo wa kidini wa mgombea unatazamwa na wapiga kura wengi kuwa
kigezo muhimu.
1 kati ya wamarekani 5 ni wakatoliki.
Papa Francis ni maarufu sana nchini Marekani.
No comments:
Post a Comment