Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Mkutano
wa Mwaka wa 25 wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF
uliobeba kauli mbiu ya "Uendeshaji wa sekta ya hifadhi ya jamii na
umuhimu wa kuzingatia mabadiliko", Naibu Waziri wa
Fedha na Mipango, Mh. Ashatu Kijaju akitoa hotuba yake wakati
akifungua mkutano huo uliowakutanisha Wadau mbalimbali, unaofanyika kwa
siku mbili kuanzia leo February 11 - 12, 2016 kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam. Katika
hotuba yake ya Ufunguzi huo, Mh. Kijaji ameupongeza uongozi mzima wa
PPF kwa kazi nzuri wanayoifanya katika suala zima la kuihudumia jamii,
pamoja na kuipongeza ameutaka mfuko huo kuwakumbuka Wakulima kule
vijijini kwa kuwaunganisha katika mtandao na kuwaingiza katika mfuko huo
ili nao wapate kunufaika na mafao ya uzeeni.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa mwaka wa 25 wa wanachama
na wadau wa PPF uliobeba kauli mbiu ya "Uendeshaji wa sekta ya hifadhi ya jamii na umuhimu wa kuzingatia mabadiliko", unaofanyika kwa siku mbili kuanzia leo February 11 - 12, 2016 kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa PPF, Ramadhan Kijjah
akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mh.
Ashatu Kijaju.
Baadhi ya Wadau washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Mkutano
wa Mwaka wa 25 wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa PPF uliobeba kauli
mbiu ya "Uendeshaji wa sekta ya hifadhi ya jamii na umuhimu wa
kuzingatia mabadiliko", Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mh. Ashatu Kijaju alipokuwa akifungua mkutano huo uliowakutanisha Wadau mbalimbali, unaofanyika kwa siku mbili kuanzia leo February 11 - 12, 2016 katika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam.
Meza kuu wakati mkutano ukiendelea
Mmoja wa Wadau wakubwa wa mfuko wa PPF, Bwa.Bakari Kaoneka aliyekuwa
akifanya kazi katika Ofisi ya Msajili wa Madawa akitoa ushuhuda wake
mbele ya wadau wa mfuko huo kuhusiana na namna alivyonufaika na Fao la
Uzeeni kupitia mfuko huo, Bw. Bakari ametoa angalizo kwa vijana wengi
wanaojishughulisha na kazi mbalimbali kuwa wafikirie ipo siku moja na
wao watastaafu,kwa hivyo ni lazima wajiwekee akiba ya uzeeni.
Meneja
Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele akijadiliana jambo
na baadhi ya wafanyakazi wenzake wakati wa Mkutano wa Mwaka
wa 25 wa Wanachama na Wadau wa Mfuko wa PPF uliobeba kauli mbiu ya
"Uendeshaji wa sekta ya hifadhi ya jamii na umuhimu wa kuzingatia
mabadiliko", unaofanyika kwa siku mbili kuanzia leo February 11 - 12, 2016 katika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam.
Mmoja
wa wanachama wa Mfuko wa PPF mwenye ulemavu wa kusikia akiendelea
kufatilia mada mbali mbali kwenye mkutano huo kupitia mkalimani wa lugha
ya alama.
Wadau wakipitia kablasha la PPF.
Picha ya pamoja na washindi wa Tuzo mbali mbali zilizotolewa na Mfuko wa PPF.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa GEPF, Daud Msangi akitoa hotuba fypi ya shukrani kwa niaba ya mifuko ya hifadhi za jamii nchini.
Sehemu ya washiriki wa mkutano
wa mwaka wa 25 wa wanachama na wadau wa Mfuko wa PPF uliobeba kauli
mbiu ya "Uendeshaji wa sekta ya hifadhi ya jamii na umuhimu wa
kuzingatia mabadiliko", ulioanza leo kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa
Mikutano wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment