Taasisi ya TANZANIA WOMEN OF ACHIEVEMENT (TWA) imetangaza uzinduzi wa kampeni ya uwiano wa kijinsia kwenye kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani ya Wanawake inayotoa wito kwa kila mtu kuchukua hatua za dhati kusaidia upatikanaji wa usawa wa jinsia kwa kasi zaidi ili kuwasaidia wanawake na wasichana kufikia malengo yao.
Mwenyekiti
wa Taasisi ya TANZANIA WOMEN OF ACHIEVEMENT (TWA), Sadaka Gandi
akifafanua jambo kuhusu uzinduzi wa kampeni ya usawa wa kijinsia kwenye
mkutano na waaandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es salaam.
Hali
kadhalika inatoa wito kwa jamii kuwa na uongozi ulio na usawa wa
kijinsia, kuheshimu na kuthamini tofauti bainia ya jinsia, kuanzisha
utamaduni jumuishi na kuondoa upendeleo kwenye sehemu za kazi.
Akizungumza
kwenye mkutano wa waandishi wa habari kwenye ofisi za TWA jijini Dar es
Salaam Rais wa TWA, Bi. Irene Kiwia alisema kuwa lengo la Kampeni ya
Uwiano wa Kijinsia ni kutoa wito kwa wanawake na wanaume kuungana
pamoja kusaidia wanawake kufikia hali ya usawa kwa idadi kubwa na
kutambua mchango wao usio na ukomo wanaoutoa kwenye uchumi duniani kote
kwa ujumla hususani nchini kwetu Tanzania.
“Kampeni
ya Uwiano wa Kijinsia inamaanisha kutoa wito kwa wadau wote vikiwemo
vyombo vya habari, watu binafsi, serikali na mashirika yote kutambua na
kujenga uelewa kuhusu mianya inayozuia mchakato wa kuwepo usawa wa
kijinsia na kutaka kuchukua hatua za dhati kuharakisha mabadiliko,”
alisema Kiwia.
“Mwaka
2014 Jukwaa la Uchumi Duniani (World Economic Forum -WEF) lilitabiri
kuwa usawa wa jinsia duniani utafikiwa mwaka 2095. Lakini mwaka mmoja
baadaye, yaani 2015 lilikadiria kuporomoka kwa hatua husika na kupunguza
kasi ya kufikia uwiano kuwa pengo la kijinsia linaweza kuzibwa ifikapo
mwaka 2133. Hii inamaanisha kusubiri kwa miaka 117 ambayo ni mingi sana.
Kutokana na hali hiyo TWA inaungana na wito wa dunia wa kuitaka kila
nchi kuliweka suala la jinsia kwenye ajenda zake na kuharakisha kasi ya
kufikia lengo la usawa wa kijinsia .” alisema Kiwia.
Waandishi
wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakisikiliza kwa makini
maelezo kutoka kwa Rais wa TWA, Irene Kiwia kuhusu uzinduzi wa kampeni
ya usawa wa kijinsia katika mkutano uliofanyika jana Jijini Dar es
salaam.
Akitoa
wito kwa watu binafsi, mashirika na wadau wengine kushiriki kwenye
kampeni hiyo Mwenyekiti wa TWA Bi. Sadaka Gandi alisema Kampeni
itahusisha matembezi ya kilomita sita asubuhi ya siku ya tarehe Tano
mwezi March kuanzia kwenye `Viwanja vya Mbio za Mbuzi´ maarufu kama
‘Uwanja wa Farasi’ kupitia kwenye makutano ya Shule ya Kimataifa ya
Tanganyika (IST), kuelekea Kanisa Katoliki la Mt. Petro na kupitia
Ubalozi wa Kenya nchini na kurudia sehemu yalipoanzia.
Bi.
Sadaka Gandi aliendelea kusema kuwa matembezi hayo yatafuatiwa na
mkutano wa kusherehekea siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani ambao
utafanyika Machi 6, 2016 kwenye Hoteli ya Regency Kilimanjaro.
Bibi
Gandi alisema, “Mkutano huu utawakutanisha wanawake na wanaume kutoka
sehemu tofauti ambao watashirikiana na kushawishiana kuungana na
harakati hizi, vile vile tutaonyesha mafanikio yaliyopatikana mpaka sasa
kutoka Mkutano wa Beijing miaka 21 iliyopita, na hali kadhalika ni
kasoro gani ambazo bado zipo na ni kwa namna gani ushirikiano wa pamoja
unaweza kuharakisha mabadiliko. Tunaamini mchango wako sio tu kwamba
utachangia msingi wa maendeleo ya wanawake bali pia utaonesha ni jinsi
gani kampuni yako inachangia kwenye upatikanani wa usawa wa kijinsia
kwa ujumla”.
Bibi
Gandi alisema kuwa mkutano huo utazungumzia masuala mbalimbali
yanayomhusu mwanamke kwa kuzingatia elimu, afya, uongozi, haki na sheria
na uchumi.
“Usawa
wa jinsia ni muhimu kwa sababu umefungamana na kukua kwa uchumi kwani
maendeleo ya wanawake na uongozi ni nguzo ya ufanisi kwenye biashara na
ustawi wa uchumi”, alihitimisha.
No comments:
Post a Comment