TWIGA
mwangavu aliyepewa jina la Omo ameonekana akivinjari katika Hifadhi ya
Taifa ya Tarangire wilayani Monduli mkoani Arusha akiwa na kundi la
wenzake ambalo halikuonekana kumshangaa kutokana na kutofautiana nao.
Mwanajiolojia
Dk. Derek Lee, mwanzilishi na mwanasayansi katika Taasisi ya Mazingira
Asili, ndiye aliyembaini twiga huyo mwang’avu.
Derek(45),
alisema: ‘Hali ya Omo kwa kitaalamu hujulikana kama ‘leucistic’,
akimanisha sehemu kubwa ya seli za ngozi yake hazina uwezo wa
kutengeneza rangi lakini baadhi zina uwezo huo na ndiyo maana yu
mwangavu na macho mekundu au bluu kama walivyo binadamu albino.
“Hata
hivyo twiga huyo si albino, bali kama tulivyoona ni leucism, ambayo
licha ya kuchangia macho mekundu au bluu kama albino, huwa na ngozi
nyeupe angavu wakati albino ni weupe kamili.
“Hii
ni hali ya kinasaba,” ‘Omo ni twiga pekee mweupe ambaye hadi sasa
tunamfahamu, lakini tumewahi kuona wanyama wenye hali kama yake wakiwamo
kongoni, nyati na mbuni katika Hifadhi ya Tarangire’.
Aliongeza:
‘Omo anaonekana kuzoeana na twiga wengine, daima amekuwa akionekana
akiwa na kundi kubwa la twiga wa rangi ya kawaida ambalo halionekani
kujali utofauti wake wa rangi.
‘Omo
kwa sasa ana umri wa miezi 15, akiwa amefanikiwa kupita mwaka wake wa
kwanza kama twiga mtoto kipindi ambacho ni hatari zaidi kwa twiga wadogo
kutokana kuwindwa mno na wanyama wakali wala nyama kama vile simba,
chui na fisi.
‘Fursa
yake ya kuendelea kuishi ni kubwa lakini twiga wakubwa mara kwa mara
hukumbana na ujangili unaolenga nyama ya pori na rangi yake ya ajabu
inaweza kuwa kivutio zaidi kwa majangili.
“Sisi
na washirika wetu tunafanya kazi kwa ajili ya uhifadhi wa twiga na
shughuli za kupinga vitendo vya ujangili, ambazo zitamsaidia Omo na
wenzake fursa nzuri ya kuishi miaka mingi ya kawaida.
‘Tuna
matumaini ataishi maisha marefu na siku moja atazaa watoto wake.’
Taasisi hiyo inafanya utafiti wa sayansi kutoa elimu kwa umma na
harakati za ushawishi juu ya kutunza uasili.
Inaendesha
mradi mkubwa zaidi kuwahi kufanywa wa utafiti wa twiga, kutambua kila
twiga aliyepo na kuandika ripoti ya maisha ya twiga zaidi ya 2,100
wanaoishi katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire.
CHANZO: MTANZANIA.
No comments:
Post a Comment