Serikali
ameiagiza bodi ya utalii nchini TTB kuvitangaza vivutio vya utalii vya
TANZANIA kwenye vyombo vya habari vya kimataifa ili idadi ya watalii wa
kutoka nje waweze kuongezeka na kufikia milioni tatu katika kipindi cha
miaka miwili ijayo
Kamimu Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Bi Devota
Mdachi akitoa taarifa ya masuala mbalimbali yahusuyo Bodi yake mbele ya
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Profesa Jumanne Maghembe wakati wa
mkutano na Menejimenti ya TTB.
Serikali ameiagiza bodi ya utalii nchini TTB kuvitangaza
vivutio vya utalii vya TANZANIA kwenye vyombo vya habari vya kimataifa
ili idadi ya watalii wa kutoka nje waweze kuongezeka na kufikia milioni
tatu katika kipindi cha miaka miwili ijayo.
Akizungumza na watendaji wa bodi ya watalii jijini DSM Waziri wa
maliasili na utalii Profesa JUMANNE MAGHEMBE amesema TTB ijiwekee
mikakati ya kutangaza mbuga za wanyama na fukwe za bahari ili vifahamike
kote ulimwenguni.
Naye kaimu mkurugenzi mkuu wa TTB, DEVOTA MDACHI amesema watatangaza
vivutio hivyo katika vyombo vya BBC, CNN na vyombo vya ndani kwa
kushirikisha wadau wengine wa utalii.
No comments:
Post a Comment